Friday, 11 December 2015

SPURS ,DORTMUND ZAPENYA '32 BORA" EUROPA

Erik Lamela
Tottenham Hotspur nayo imesonga mbele baada ya ushindi wa 4-1 dhidi ya Monaco katika mchezo wa Kundi J, nyota wake Erik Lamela akifunga mabao matatu peke yake dakika za pili, 15 na 37, bao lingine likifungwa na Tom Carroll dakika ya 77, huku la wapinzani likifungwa na Stephan El Shaarawy dakika ya 61 Uwanja wa White Hart Lane.
Spurs inamaliza kileleni mwa kundi hilo kwa pointi zake 13 mbele ya RSC Anderlecht, ambayo jana imeifunga 2-1 FK Qarabag na kumaliza na pointi 10.

 
 
Borussia Dortmund nayo imesonga mbele licha ya kuchapwa 1-0 nyumbani na PAOK Salonika katika mchezo wa Kundi C jana Uwanja wa Signal Iduna Park, bao pekee la Robert Mak dakika ya 33.
Borussia Dortmund inamaliza na pointi 10, nyuma ya FK Krasnodar, ambayo jana imeshinda 3-0 ugenini dhidi ya FK Qabala, mabao yake yakifungwa na Ragnar Sigurdsson, Mauricio Pereyra na Wanderson do Carmo Carneiro Uwanja wa Bakcell Arena, hivyo kumaliza na pointi 13.
Timu zilizosonga mbele ni Molde, Fenerbahce, Liverpool, FC Sion, FK Krasnodar, Borussia Dortmund, Napoli, FC Midtjylland, SK Rapid Wien, Villarreal, Sporting Braga, Marseille, Lazio, St Etienne, Lokomotiv Moscow, Sporting Lisbon, FC Basel, Fiorentina, Tottenham Hotspur, RSC Anderlecht, FC Schalke 04, Sparta Prague, Athletic Club na FC Augsburg ambazo zinaunagana na Shakhtar Donetsk, Manchester United, Galatasaray, Sevilla, Bayer 04 Leverkusen, Olympiakos, FC Porto na Valencia CF zilizotolewa Ligi ya Mabingwa.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA