Sunday 27 December 2015

PICHA:MASHABIKI WA MBEYA CITY WAKIMDUNDA SHABIKI WA YANGA KAMA MWIZI


Mashabiki wa Mbeya City jana waliamua kulipa kisasi wakati timu yao ilipokuwa ikiadhiwa na Yanga uwanjani kwa kumtandika kinoma shabiki mmoja wa Yanga.


Mashabiki hao wa Mbeya City waliokuwa wamekaa upande wao, lakini shabiki wa Yanga akawafuata na kuanza kuwakejeli, walimtandika kiasi cha kuanguka naye chini.

Pamoja na kuanguka, waliendelea kumtandika hadi askari polisi walipoingilia na kumuondoa katika eneo hilo huku wakimlaumu kuwafuata mashabiki hao waliokuwa wamekaa upande ambao haukuwa na mashabiki wa Yanga.


Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara, Yanga iliitandika Mbeya City kwa mabao 3-0 huku beki wake Tumba Sued akilambwa kadi ya nyekundu kwa kumtandika kibao Donald Ngoma.
credit- Salehjembe 

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA