Friday 18 December 2015

YANGA SC WALALAMIKIA KUCHEZESHWA LIGI KUU WAKATI SIMBA NA AZAM FC HAWACHEZI


Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro amezungumza na Waandishi wa Habari leo

Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
YANGA SC imelalamikia kuchezeshwa mfululizo mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, wakati wapinzani wao, Azam FC na Simba SC hawachezi.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro amewaambia Waandishi wa Habari katika Mkutano uliofanyika makao makuu ya klabu Jangwani, Dar es Salaam kwamba hawapendezewi na mwenendo huo.  
“Tunakwenda kucheza kesho na Stand United, lakini wenzetu bado wana viporo na hawachezi. Hizi ni figisu, ilifaa wote tucheze pamoja.
Wakiendelea kufanya hivi, tutatumbua majipu,”. “Kwa nini tuachiwe sisi tu tucheze wakati wenzetu wakae watutazame, si jambo zuri. Tuwaombe wenye kusimamia kanuni na sheria za mpira Tanzania waliangalie hili,”amesema Muro.
Yanga SC inatarajiwa kushuka dimbani kesho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kumenyana na Stand United ya Shinyanga ukiwa ni mchezo wa tatu ndani ya siku 10, baada ya Jumamosi iliyopita kutoa sare ya 0-0 na Mgambo JKT na Jumatano kushinda 1-0 dhidi ya African Sports Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. 
Wapinzani wa Yanga SC katika mbio za ubingwa, Azam FC walimenyana baina yao Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kutoa sare ya 2-2, lakini katikati ya wiki walikuwa mapumzikoni, ingawa kesho nao watakuwa kazini tena.
Azam FC watakuwa Uwanja wa Majimaji Songea kumenyana na wenyeji, Majimaji wakati Simba SC watakuwa wageni wa Toto Africans Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza. 
RATIBA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
; Desemba 19, 2015
Yanga SC vs Stand United
Mwadui FC vs Ndanda FC
Kagera Sugar vs African Sports
Prisons         vs Mtibwa Sugar
Toto Africans vs Simba SC
Majimaji         vs Azam FC
Desemba 20, 2015
JKT Ruvu vs Coastal Union

Mbeya City vs Mgambo JKT

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA