AL-SHABAB WAKO 'HURU' KUSHIRIKI SOKA SOMALIA
Wapiganaji wa Alshabaab
Mkuu wa
shirikisho la soka nchini Somalia amesema kuwa kundi la wapiganaji wa
al-Shabab liko huru kushiriki katika ligi kuu ya soka nchini humo.
Abdiqani
Said Arab amemuambiwa mwandishi wa BBC jijini Nairobi John Nene kwamba
iwapo wapiganaji hao wanataka kushiriki watepewa fursa.
''Hatuwapingi na hawatupingi," alisema.
Kundi la
al-Shabab linaloendesha itikadi kali, limewaagiza wanasoka kuvaa suruali
ndefu na limepiga marufuku muziki katika maeneo linalodhibiti.
Hata
hivyo, Bw Arab amesema kuwa anaamini kwamba wafuasi wa kundi hilo
wanahudhuria mechi za soka lakini akakataa kutoa maelezo zaidi.
Soka Somalia
Mwezi Uliopita,mechi moja nchini Somalia ilipeperushwa moja kwa moja katika runinga ya kitaifa kwa mara ya kwanza.
''Ligi hiyo inawavutia wachezaji wa kigeni kutokana na hali shwari ya usalama'',alisema Bw Arab.
''Zaidi ya wachezaji 20 wa kigeni wanashiriki katika ligi yetu," katika vilabu 6, aliongezea.
Vikosi
vya Umoja wa Afrika vinavyoungwa mkono na serikali vimeimarisha udhibiti
wao wa maeneo mengi yaliokuwa yakidhibitiwa na kundi hilo ambalo
linapigana kuweka utawala wa kiislamu.BBC
0 comments:
Post a Comment