JE WEWE NI MSIKILIZAJI MZURI WA MUZIKI? HII INAKUHUSU ,SOMA UJIELIMISHE
Muziki uko kila mahali tunapoenda,
iwe umeusikia kupitia redio,
katika mgahawa, nyumba za ibada au katika maeneo ya starehe.
Hakuna utafiti wowote uliowahi kufanywa ambao uliweza kuthibitisha madhara yanayotokana na mtu kusikiliza muziki,
ila tafiti nyingi zimeegemea katika kutoa faida za muziki katika maisha yetu ya kila siku.
Haijalishi aina gani ya muziki unaipenda sana kusikiliza ilimradi unaupenda utakusaidia kitu tu.
Hebu tuangalie faida japo chache ambazo zinaletwa na kusikiliza muziki.
1.KUTUNZA KUMBUKUMBU
Haijalishi
sasa hivi una umri gani lakini kila mara kuna wimbo ukiusikia lazima
utakukumbusha matukio yaliyopita ambapo wakati unapitia kipindi hicho
wimbo huo ndio ulikuwa unapigwa.
Na utajikuta unaanza kufurahi na kuzidi kuziimarisha kumbukumbu zako za matukio ya zamani.
Si kitu cha ajabu kumsikia mtu akisikia wimbo fulani unaanza kusema "Aah! wimbo wangu huo!"
2.KUIMARISHA UMAKINI
Ukiwa
ni msikilizaji mzuri wa nyimbo mara nyingi unatengeneza tabia ya
kusikiliza wimbo kuanzia mashairi hadi midundo yake na hii si kazi
rahisi hata kidogo kwani unatakiwa umakini wa hali ya juu kufanya jambo
hili.
Cha ajabu utamkuta mtu anaupenda wimbo lakini hajui hata mashairi yanazungumzia nini,
tabia
itakufanya hata uwezo wako wa kusikiliza mtu anapoongea uwe mdogo kwani
kitendo cha kusikiliza na kutafsiri papo kwa papo kina umuhimu sana
katika ulimwengu wa kujifunza.
3.HULETA HISIA ZA UTULIVU
Muziki sio lazima uwe na midundo,
lakini hata mashairi tupu yanaweza kukuletea utulivu unaoufanya ubongo upumzike vizuri.
Na ndio maana unapomuimbia mtoto mdogo hachelewi kulala.
Na
watu wazima mara nyingi husinzia na kupumzika haraka wanaposiliza
nyimbo za taratibu kwani ndizo ambazo zinaupa ubongo hisia nzuri kwa
muda huo.
4.HUONGEZA NGUVU WAKATI WA SHUGHULI
Mathalani
unapokuwa unafanya shughuli fulani ambayo ni kutumia nguvu nyingi
muziki husaidia kuongeza utendaji kazi wako muda huo.
Na
ndio maana hata washauri wa mazoezi wanapenda kuwaeleza wateja wao
wanapofanya mazoezi ya kukimbia au yoyote ya kutumia viungo ni vyema
wakaweka muziki ambao utakuwa unawasindikiza ili wasichoke haraka.
5.UNAONGEZA MANENO
Hata kama wewe ni mtumiaji mzuri wa lugha yako lakini kuna maneno unaweza ukawa hujawahi hata kuyatumia katika maisha yako.
Sasa unapokuwa msikilizaji mzuri wa mashairi ya nyimboi inakusaidia kuongeza maneno na maana zake.
6.CHANGAMOTO ZA UWEZO WA KUHOJI
Muziki mara zote kama unausikiliza kwa makini unakuletea changamoto za kujiuliza kama kinachoimbwa ni sawa au sio sawa.
Na kitu pekee kitakachokupa uwezo wa kutambua hilo ni uwezo wako wa kuhoji mashairi kutokana na tafsiri yako uliyopata.
Na ndio maana sitashangaa kumkuta mtu anaimba mashairi ya lugha yake lakini hajui hata aliyeimba alikuwa ana maanisha nini.
7.KUTIA HAMASA
Mara kwa mara si kitu cha ajabu kukuta unasikiliza wimbo ambao mashairi yake yanakugusa moja kwa moja,
na bahati nzuri anatoa na suluhisho la tatizo humo humo.
Na hali hiyo itakufanya ujione hauko peke yako mwenye hisia kama hizo hivyo kukutia hamasa ya kusonga kusonga mbele.
Na ndio maana kuna nyimbo kuzisahau kwako inakuwa ni ndoto kwani katika kipindi fulani cha maisha yako ulikugusa kiukweli.
8.HUONGEZA UBUNIFU
Muziki wenyewe tu ni kazi ya ubunifu kuanzia melodi ya mashairi hadi midundo yake.
Japo
si kila msikilizaji wa muziki anaweza kuja kuwa msanii lakini utafiti
unaonyesha watu wengi waliokuja kuwa wasanii wa muziki walikuwa
wasilikzaji wazuri wa muziki.
Hata
watu wengine wanaofanya kazi nyingine za sanaa wanatumia muziki kama
chombo moja wapo cha kuwaongezea ubunifu kwa mfano waandishi, wachoraji,
wachezaji au wanaofanya kazi za kutumia umakini mkubwa wa ubongo.
9.HUBADILISHA HALI YA UBONGO
Muziki unaweza ukakusaidia kubadilisha hali unayojisikia iwe ya huzuni, mawazo, upweke, hofu au hata hasira.
Na
ndio maana wataalamu wanashauri ikiwa uko na hali mojawapo nilizozitaja
hapo juu uwe unatumia njia ya kuimba nyimbo unazozipenda kukurudisha
katika hali yako ya kawaida.
10.HUONGEZA UFANISI WA KAZI
Haijalishi kazi gani unayofanya,
ukimya utakufanya akili yako ihamie kwingine ambako utaufanya ubongo upoteze umakini na shughuli unayofanya muda huo.
Ila kwa kutumia aina ya muziki unaoupenda utaifanya akili ijisikie vizuri na hata kuzuia kuchoka haraka.
NAJUA KUNA WATU SI WAPENZI WA KUSIKILIZA MUZIKI KABISA.
NA
MAKALA HII HAIPO KWA AJILI YA KUKUSHAWISHI UANZE TABIA AMBAYO HUKUWAHI
KUWA NAYO KABLA ILA IPO KWA AJILI YA WALE WAPENZI WA MUZIKI ILI WAUTUMIE
MUZIKI HUO KATIKA KUBORESHA SHUGHULI ZAO.
0 comments:
Post a Comment