SERIKALI IMENUNUA MASHINE MPYA YA CT-SCAN KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI
Na Magreth Kinabo –MAELEZO
Serikali
imenunua mashine mpya ya CT-Scan yenye thamani ya takriban dola za
Marekani milioni 1.7 yenye uwezo wa hali ya juu kwa ajili ya kutoa
huduma za uchunguzi wa magonjwa mbalimbali katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili(MNH) iliyopo jijini Dar es Salaam.
Ununuzi
wa mashine hiyo, umefanyika kufuatia agizo la Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliyoifanya hivi
karibuni ambapo aliutaka uongozi wa hospitali hiyo kuboresha huduma zake
na kuhakikisha vifaa tiba na dawa vinapatikana ili kuhakikisha
Watanzania wanapata huduma bora za afya.
Hayo
yamegundulika leo baada ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangala aliyoifanya leo katika
hospitali hiyo, ambapo alitembea Idara ya Magonjwa ya Dharura,Idara ya
Mionzi, sehemu mpya ya wagonjwa waliopo chini ya ungalizi maalum(ICU),
ambayo inafanyiwa ukarabati na wodi mojawapo.
Naibu Waziri akitembelea katika Idara ya Mionzi ambapo alijionea mashine za MRI na CT –Scan zinavyofanyakazi.
Akizungumzia
kuhusu mashine ya CT-Scan Mkuu wa Idara ya Mionzi, Dkt. Flora Lwakatare
alisema mashine hiyo , iliyotengenezwa na kampuni ya Siemens mpya
imefungwa siku mbili zilizopita na imeshaanza kufanya majaribio kwa
wagonjwa 26 tangu ilipofungwa
Dkt.
Flora aliongeza kwamba mashine hiyo iko moja tu nchini na katika nchi za
Afrika Mashariki nchi nyingine iliyonunua mashine hiyo ni Kenya katika
Hospitali ya Aghakhan.
“ Mashine
hii inatoa huduma za hali ya juu kwa magonjwa ya moyo, ubongo tumbo
kifua na inauwezo wa kupima kifua na tumbo kwa sekunde sita,” alisema.
Akizungumzia kuhusu mashine hiyo Naibu Waziri huyo, alisema imenunuliwa kwa fedha za Serikali wala sio mkopo.
“Tunatarajia kununua mashine hii katika hospitali ya Dodoma na Mwanza,” alisema Waziri Kingwangala.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi wa MNH, Profesa Laurence Maseru alisema
mashine hiyo ina sahani 128 mara 2 ikilinganishwa na iliyokuwepo ambayo
ilikuwa inatumia sahani sita.
Kwa
upande wa mashine ya MRI ambayo tangu ilipofanyiwa matengenezo makubwa
Novemba 26, mwaka jana hadi sasa imesha hudumia wagonjwa 560.
Dkt.
Kingwangala alitembea katika Idara cha huduma za dharura na kuangalia
jinsi huduma zinavyotolewa, ambapo alielezwa na Mkuu wa Idara ya
Magonjwa ya Dharura Dkt. Juma Mfinaga alisema ambayo huhudumia wastani
wa wagonjwa 300 hadi 400 kwa siku ambacho kinafanya kazi kwa kutumia
mfumo maalum wa kompyuta bila kutumia karatasi.
Naibu
Waziri huyo, mbali na kupongeza maboresho yaliyofanyika na huduma nzuri,
alitoa maagizo kwa uongozi wa hospitali hiyo kuboresha huduma za
zilinazotolewa hospitalini kuwa za kitaifa zaidi.
Alitolea mfano huduma kulipa kwa kuongeza vitanda na matumizi ya choo kimoja kila chumba ili kuweza kuvutia wateja.
“Sisi
tunaweza kufanya biashara kwa kuboresha huduma za kulipa ili zimpendeze
na kuvutia wateja. Na fedha zitakazopatikana zitatumika kununua dawa ,
vifaa tiba na kuwapatia wafanyakazi motisha, alisema.
Aliutaka
uongozi huo pia kuhakikisha inawalipa wafanyakazi fedha za malipo ya
ziada kwa wakati ifikapo tarehe 25 ya mwezi unaofuata,kutumia mfumo wa
kompyuta sehemu zote, kupunguza msongamno wa wagonjwa na kuwa wabunifu.
0 comments:
Post a Comment