GUARDIOLA ASAINI RASMI KUINOA MANCHESTER CITY 2016-2017
KOCHA
Pep Guardiola amesaini Mkataba wa miaka mitatu kuifundisha Manchester
City baada ya kuthibitishwa Manuel Pellegrini ataondoka Etihad mwishoni
mwa msimu.
Pellegrini
alifichua habari hizo katika Mkutano na Waandishi wa Habari leo
kuelekea mchezo dhidi ya Sunderland kesho, wakati City imesema imekuwa
ikimuhitaji Guardiola tangu mwaka 2012.
City imekuwa ikiendesha kwa siri mipango ya kumchukua kocha impendaye, Guardiola kabla ya leo kuweka wazi atajiunga na timu.
Pep Guardiola amesaini Mkataba wa miaka mitatu kujiunga na Manchester City msimu ujao
Pellegrini amesema klabu haitaendelea naye baada ya kumakliza msimu na tayari kocha mpya amepatikana.
Taarifa
ya Man City imesema; "Manchester City inaweza kuthibitisha kwamba
katika wiki za karibuni imekuwa ikishughulikia kukamilisha Mkataba na
Pep Guardiola awe kocha Mkuu wa MCFC kwa msimu wa 2016/17 wa Ligi Kuu ya
England kuendelea.
"Mkataba ni wa miaka mitatu. Majadiliano hayo ni matokeo mijadala ya mwaka 2012. Kwa heshima yetu kwa Manuel Pellegrini na wachezaji, klabu inataka kuweka wazi uamuzi wake kwa jamii ili kuzuia tetesi zisizo za kawaida.
Sasa
Pellegrini ataendelea na kazi Manchester City hadi mwishoni mwa msimu
kabla ya kumpisha kocha mpya, Guardiola ambaye kwa sasa anafundisha
Bayern Munich ya Ujerumani iliyomchukua kutoka Barcelona ya Hispania.
Manuel Pellegrini amethibitisha ataondoka Manchester City mwishoni mwa msimu kumpisha Guardiola
0 comments:
Post a Comment