Friday, 5 February 2016

Kauli ya Lowassa kuhusu uchaguzi wa marejeo Zanzibar


Edward Lowassa akizungumza na wazee wa CHADEMA Jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam jana
Aliyekuwa Mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, Edward Lowassa, akizungumza na wazee wa chama hicho, jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam jana walipomtembelea ofisini kwake amewataka wazee hao kutokata tamaa na kujipanga kimkakati kujiandaa na kuimarisha chama chao pamoja na ukawa kwa ujuml ili kujiandaana uchaguzi ujao wa 2020.
Lowassa pia ameendelea kuwataka Watanzania kuwa watulivu na kulinda amani ya nchi na kujiepusha na kila jamboambalo wanaona linamwelekeo wa uvunjifu wa amani.
Hayo aliyasema wakati alipokuwa akijadili mambo mbalimbali ya kuimarisha chama.
Aidha, aliwaomba wazee hao kutokata tamaa kwani kuna mambo mengi ya kufanya hadi kufikia malengo waliyojiwekea.
"Hali ya chama chetu na UKAWA iko vizuri, uchaguzi tulishinda, sisi tunajua, Jumuiya za Kimataifa zinajua na hata CCM wenyewe wanajua kama tulishinda, ila ubabe wao na dhuulma ndio wamefanya waliyofanya," alisema.
Lowassa alifafanua zaidi kuwa kama chama kinachojiandaa kushika dola hawakuwa tayari kuingia Ikulu kwa damu ya watazania na ndiyo maana hata vijana walipomtaka atoe kauli ya kuingia barabarani anasema, "niliwazuia."


Kuhusu suala la mgogoro wa kisiasa na kutangazwa tareye ya marejeo ya uchaguzi Zanzibar, Lowassa amewataka CCM kuacha kufanya siasa za kiimla na kuwa wasijidanganye kwamba Zanzibar ikichafuka, Bara itasalimika.Lowassa amesema ni vema serikali ikahakikisha inapata suluhu ya mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio Machi 20 mwaka huu.
Lowassa amesema anaunga mkono uongozi wa CUF kutokushiriki uchaguzi huo huku akisisitiza endapo serikali ikishindwa kumaliza mgogoro huo kabla ya Machi 20 mwaka huu, huenda hali ya kisiasa Zanzibar ikabadilika. 
Aidha, amemshukuru Waziri Mkuu kwa kuruhusu mikutano ya kisiasa, suala ambalo linawapa fursa ya kuajipanga ili kuwashukuru watanzania waliojitokeza kupiga kura Oktoba 25, 2015. 

Risala ya wazee hao iliyosomwa na mzee Enock Ngombare imempongeza Lowassa kwa na uvumilivu wake baada ya uchaguzi, ambapo pia wamemhakikishia kuwa wako pamoja naye katika safari ya kuelekea mwaka 2020. 
Katika mkutano huo pia uliohudhuliwa na kada wa siku nyingi Kingunge Ngombare Mwiru, Lowassa amewataka Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla kuwa watulivu na kuhakikisha wanadumisha amani ya nchi hasa katika kipindi hiki ambacho viongozi wanaendelea na juhudi za kutafuta suluhu ya kisiasa visiwani Zanzibar.

Mmoja wa wazee hao akitoa mawazo yake juu ya namna ya kufanya kabla hawajaingia katika uchaguzi mwingine ili kukabiliana na mbinu za chama ha mapinduzi ili kuwashinda kwenye majimbo mengi zaidi ya sasa.

Mze Enock Ngombale, Ndugu wa Mze Kingunge Ngombale Mwiru ambaye ni Mwenyekiti wa Wazee wa Chadema jimbo la Ubungo, akiwasilisha mipango na mikakati ya Chama hicho kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2020.


0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA