MANCHESTER CITY BINGWA CAPITAL ONE CUP,
MANCHESTER
imetwaa Kombe la Ligi England, maarufu kama Capital One Cup baada ya
kuifunga kwa penalti 3-1 Liverpool Uwanja wa Wembley kufuatia
sare ya 1-1 ndani ya dakika 120.
Shujaa
wa Man City leo alikuwa ni kipa Willy Caballero aliyeokoa penalti tatu
na kukipa taji la Capital One kikosi cha Manuel Pellegrini, baada ya
kiungo Yaya Toure kufunga penalti ya mwisho.
Emre Can pekee alifunga penalti ya Liverpool, wakati za Lucas, Philippe Coutinho na Adam Lallana zilichezwa na Caballero, huku za City zikitiwa nyavuni na Sergio Aguero, Jesus Navas na Toure, baada ya Fernandinho kukosa ya kwanza.
Willy Caballero akiwa amebebwa na wachezaji wenzake wa Manchester City baada ya kuokoa penalti tatu na kuipa timu hiyo taji la Capital One Uwanja wa Wembley
0 comments:
Post a Comment