MBWANA SAMATTA AANZA KUWASHA MOTO UBELGIJI
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta
amefunga bao lake la kwanza katika klabu yake mpya, KRC Genk katika
mchezo wa Ligi Kuu ya Ubelgiji wakishinda 3-2 dhidi ya Club Bruge Uwanja
wa Cristal Arena, Genk.
Samatta
aliyejiunga na Genk Januari akitokea TP Mazembe ya DRC, alifunga bao
hilo dakika ya 81 akimalizia pasi ya kiungo Ruslan Malinovskiy, baada ya
kuingia kutokea benchi kuchukua nafasi ya Nikolaos Karelis dakika ya
79.
Na
Samatta aliyekuwa akicheza mechi yake ya tatu leo tangu ajiunge na
Genk, angeweza kufunga tena kama kama si shuti lake kupanguliwa na kipa
wa Bruge mwishoni kabisa mwa mchezo.
Mabao
mengine ya Genk yamefungwa na Karelis kwa penalti dakika ya 36 na
Thomas Buffel dakika ya 50, wakati ya Bruge yamefungwa na Thomas Meunier
dakika ya 15 na Hans Vanaken dakika ya 83.
Na
ushindi huo, unaifanya Genk ifikishe pointi 45 baada ya kucheza mechi
28 na kuendelea kukamata nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya
Ubelgiji.
0 comments:
Post a Comment