Sunday, 7 February 2016

MISS ALBINISM KANDA YA ZIWA 2016 HUYU HAPA

Mlimbwende Zawadi Dotto (pichani) ameibuka kidedea katika Mashindano ya Miss Albinism Kanda ya Ziwa yaliyofanyika usiku wa kuamkia leo jijini Mwanza. 
Miss Zawadi mwenye umri wa miaka 17 (mwanafunzi) ameibuka mshindi katika Mashindano hayo ambayo ni maalum kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi ii kuonyesha umahiri wao katika tasnia ya ulimbwene hii ikiwa pia ni ishara ya kwamba watu wenye ulemavu wa ngozi wanaweza kushiriki katika shughuli na mashindano mbalimbali.
Mashindano hayo yanaandaliwa na Taasisi ya kusaidia watu wanaoishi katika mazingira hatarishi iitwayo SAVE VUNERABLE FOUNDATION ya jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa shirika hilo, Alexander Exaud Mutowo ametanabaisha kwamba, baada ya mashindano hayo kukamilika kwa kanda zote nchini, washindi wa kanda hizo watashindanishwa jijini Dar es Salaam ili kumpata mshindi wa kitaifa wa MISS ALBINISM 2016.
Wshiriki Saba wa Miss Albinism 2016 Kanda ya Ziwa na umri wao katika mabano ambapo kutoka Kushoto ni Hajra Sadru (22), Antonia Mathias William (17), Furaha Edward John (17), Pendo Faustine (15), Zabibu Abdallah (18), Zawadi Dotto (17) pamoja na Asteria Christopher.
Washiriki walioingia Nne Bora ambapo kutoka kushoto ni Hajra Sadru, Furaha Edward, Zabibu Abdallah na Zawadi Dotto.
Baada ya mtifuano mkali hatimaye majaji wakatangaza washindi. Furaha Edward mshindi wa tatu (kushoto), Hajru Sadru mshindi wa pili (katikati) na Zawadi Dotto akaibuka kuwa mshindi wa kwanza (aliyepiga magoti).
Mshindi wa Miss Albinism Kanda ya Ziwa akivikwa taji lake. Wa pili kulia ni Jalia Mtani ambaye alikuwa Jaji Mkuu akitaja majina ya washindi. Pembeni ni Mshereheshaji Emmanuel Shalali kutoka Sahara Media Group.
Mshindi wa Miss Albinism Kanda ya Ziwa akivikwa taji lake. Wa pili kulia ni Jalia Mtani ambaye alikuwa Jaji Mkuu akitajana Majina ya washindi. Pembeni ni Mshereheshaji Emmanuel Shalali kutoka Sahara Media Group.
Katikati ni mshindi wa kwanza, kulia mshindi wa pili na kushoto mshindi wa tatu.
Kampuni ya Visimbuzi (Ving’amuzi) ya StarTimes ilikuwa miongoni mwa makampuni yaliyosaidia kufanikisha mashindano hayo. Mwenye kinasa sauti ni Erick Makonya ambaye ni Afisa Masoko wa kampuni hiyo Kanda ya Ziwa akitaja zawadi zilizotolewa kwa washindi na kampuni hiyo ambapo mshindi wa kwanza amejinyakulia simu ya StarTimes  aina ya Solar5, mshindi wa pili simu aina ya P40 StarTimes na mshindi wa tatu amejishindia simu aina ya B27 zote zikiwa ni smartphones kutoka StarTimes.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiongozwa na Marcella Mayala ambaye ni Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana (wa tatu kushoto) akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Magesa Mulongo ambaye alikuwa mgeni rasmi, wakiwa katika picha ya pamoja na washindi.
Alexander Exaud Mutowo, Mratibu wa Shirika la VUNERABLE FOUNDATION  lililoandaa mashindano hayo akizungumza wakati wa mashindano hayo, ambapo amewasihi wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wenye ulemavu wa ngozi ikiwemo kuunga mkono juhudi za shirika hilo kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa jiko katika kituo cha kuwahifadhi watu wenye ulemavu wa ngozi Buhangija kilichopo Mkoani Shinyanga.
Fredy Samwel Kaula, Mwenyekiti wa Shirika la VUNERABLE FOUNDATION akizungumza katika mashindano hayo.
Alfredy Kapole, Mwenyekiti wa Tanzania Albinism Society TAS akizungumza wakati wa mashindano hayo.
Marcella Mayala, Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana (wa tatu kushoto) akifungua mashindano hayo ambapo amesema ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza itaendeleza ushirikiano na Shirika la VUNERABLE FOUNDATION kwa ajili ya kupata wadau wa kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu wa ngozi.
Dickson Kiringo a.k.a Mr.White ambaye ni msanii chipukizi wa muziki wa kizazi kipya akitoa burudani. Msanii Barnaba Boy aliahidi kumsaidia Mr.White ili arekodi nyimbo mbili katika studio yake ikiwa ni bure kabisa.
Msanii Barnaba Boy akitoa burudani katika Mashindano ya Miss Albinism 2016 Kanda ya Ziwa jijini Mwanza.
Majaji kutoka kushoto ni Jaji Angelina Chuma, Jaji Mkuu Jalia Mtani na Jaji Lilian Lambo.
Alfredy Kapole, Mwenyekiti wa Tanzania Albinism Society TAS (wa pili kulia) pamoja na wadau wengine wakifuatilia mashindano hayo

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA