Sunday 7 February 2016

SAMATTA AANZA NA USHINDI KRC GENK


STRAIKA wa KRC Genk inayoshiriki ligi kuu ya Ubelgiji maarufu kama Belgium Pro League, mtanzania Mbwana Samatta, leo ameanza vema kuichezea timu yake hiyo mpya ikipata ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Mouscron-Peruwelz.
Samatta aliyeingia akitokea benchi katika dakika ya 73 akichukua nafasi ya mshambuliaji Nikos Karelis hakuonyesha dalili ya ugeni wowote katika ligi hiyo licha ya kuwa amefanya mazoezi na wenzake kwa takribani wiki moja tu.


Bao la Genk liliwekwa nyavuni na straika Thomas Buffel katika dakika ya 62, dakika 12 baada ya kiungo wa Mouscron, Coulibaly kupewa kadi nyekundu. Mchezo huo pia ulishuhudia kiungo mwingine wa Mouscron, Fejsal Mulic akilimwa kadi nyekundu ya moja kwa moja katika dakika ya 74 ikiwa ni dakika tatu tu tangu aingie kuchukua nafasi ya Julian Michel.
Kwa ushindi huo Genk imepanda hadi nafasi ya tano wakiwa na pointi 38 huku ikiishusha Zulte-Waregem yenye pointi 37 ila ina mchezo mmoja mkononi. Gent wao wanaendelea kuongoza ligi wakiwa na pointi 52 wakifuatiwa na Club Brugge yenye pointi 49.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA