Sunday 24 April 2016

LEICESTER CITY YAICHAKAZA SWANSEA CITY 4-0,ARSENAL MHMH!


Timu ya Leicester City imendelea kuongoza kwa tofauti ya pointi nane baina yake na Tottenham Hotspur, baada ya kuichakaza Swansea City kwa mabao 4-0.

Leicester ikicheza bila mfungaji wao mkuu Jamie Vardy, Riyad Mahrez alikuwa wa kwanza kufunga goli, kabla ya Leonardo Ulloa kufunga la pili na la tatu.

Marc Albrighton aliyetokea benchi aliiongezea Leicester bao la nne na kuifanya timu hiyo kuhitaji pointi tano zaidi ili kutwaa kombe la ligi hiyo kwa mara ya kwanza. 
                             Leonardo Ulloa akipachika goli kwenye lango la Swansea City
Katika mchezo mwingine Timu ya Sunderland imetoka katika kundi la kushuka daraja baada ya kupata pointi moja wanayostahili kwa kutoka sare tasa dhidi ya Arsenal.

Pande zote mbili zilishuhudia zikinyimwa penati zao kwa matukio ya kushikwa mpira kwa mkono.

Katika mchezo huo Patrick van Aanholt alipiga mpira wa adhabu uliogonga mwamba wa goli la Arsenal, huku naye kipa wa Sunderland, Vito Mannone akizuia michomo ya Mesut Ozil na Alex Iwobi.
             Kipa Petr Cech akipangua moja ya mipira hatari katika lango la Arsenal

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA