Thursday 14 April 2016

MANCHESTER UNITED KUKUTANA NA EVERTON NUSU FAINALI KOMBE LA FA


Manchester United itakutana na Everton katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la FA baada ya kusakata soka safi na kuifunga West Ham United kwa mabao 2-1.

Kinda Marcus Rashford aliandika bao la kwanza, katika mchezo huo wa marudio baada ya kunasa pande la Anthony Martial na kupiga shuti la kuzungusha lililojaa wavuni na kumpita kipa wa West Ham, Darren Randolph.

Bao la pili la Manchester United lilipachikiwa na Marouane Fellaini dakika 13 baadaye baada ya naye kunasa mpira uliopigwa na Anthony Martial na kuutumbukiza kiulaini.
                       Marcus Rashford akipachika bao la kwanza kwa shuti la kiufundi 
                         Marouane Fellaini akipachika bao la pili la Manchester United

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA