Thursday 28 April 2016

MWILI WA MWANAMUZIKI PAPA WEMBA WAPOKELEWA JIJINI KINSHASA


Mwili wa Papa Wemba, ambaye ni moja ya wanamuziki bora Afrika, umewasili nchini kwao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya kufariki dunia jumapili nchini Ivory Coast.

Mamamia ya waombolezaji walikusanyika kuungojea mwili wa nyota huyo wa muziki wa rumba, ulipowasili uwanja wa ndege wa Kinshasa.

Tamasha la usiku kucha la kumuenzi lilifanyika Jijini Abidjan, Jiji ambalo Papa Wemba alianguka na kufariki dunia wakati akitumbuiza jukwaani.

Marehemu Papa Wemba atazikwa siku ya jumanne, baada ya kuugwa kwenye uwanja wa mpira katika Jiji la Kinshasa siku ya jumatatu.
                         Jeneza lililobeba mwili wa Papa Wemba likipokelewa Kinshasa
            Waombolezaji waliofika kupokea mwili wa Papa Wemba wakiangua vilio

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA