Saturday 16 April 2016

REAL MADRID YAWAPA TANO MAJIRANI ZAO GETAFE BILA YA HURUMA


Gareth Bale amefunga goli lake la 16 katika msimu huu wakati Real Madrid ikiichakaza Getafe kwa mabao 5-1 na kukwea juu pointi moja nyuma ya vinara wa La Liga timu ya Barcelona.

Matokeo hayo ni ya ushindi wa saba mfululizo kwa Real Madrid na kufufua matumaini ya kuwania taji la ligi hiyo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2012 na kusukuma mkiani Getafe.

Alikuwa Karim Benzema aliyeifanya Real iongoze na baadaye Isco akafunga goli la pili kabla ya Bale kufunga la tatu. Rodriguez alipachika bao la nne na Cristiano Ronaldo akafunga la tano.
                                                              Isco akipachika goli la pili la Real Madrid
                       Gareth Bale akipiga mpira uliojaa wavuni na kuandika bao la tatu

Mshambuliaji wa Real Madrid, Ronaldo Ronaldo (katikati) akishirikiana na Lucas Vazquez (wa pili kulia) kuwania mpira dhidi ya kipa wa Getafe, Guaita katika mchezo wa La Liga jioni ya leo Uwanja wa Coliseum Alfonso Perez.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA