Monday 2 May 2016

CHELSEA KUIPATIA UBINGWA LEICESTER CITY LEO ?


Leicester City imebakiza pointi mbili tu kuweza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya Manchester United kuiwekea ngumu katika mchezo wao ulioishia kwa sare ya 1-1 katika dimba la Old Trafford.

Hata hivyo Leicester City inaweza kuwa bingwa leo usiku iwapo timu ya Tottenham itashindwa kuifunga Chelsea kwenye mchezo utakaochezwa kwenye dimba la Stamford Bridge.

Katika mchezo huo Leicester City ilianza vibaya baada ya kukubali goli la mapema la dakika ya nane baada ya Anthony Martial kuunganisha pande la Antonio Valencia, lakini baada ya dakika tisa kupita kapteni Wes Morgan alisawazishwa kwa mpira wa kichwa.
   Anthony Martial akipiga shuti lililoandika bao la kwanza kufungwa katika mchezo huo
          Anthony Martial wakipongezana na Wes Morgan baada ya mchezo kuisha

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA