EVERTON YAMFUNGASHIA VIRAGO KOCHA ROBERTO MARTINEZ
ROBERTO MARTINEZ ametupiwa virago na Everton, uamuzi
ulioripotiwa kuchukuliwa kufutia timu yake kuchapwa mabao 3-0 na Sunderland
Jumatano, matokeo ambayo yamewathibitishia wapinzani wao hao kubaki Premier
League.
Kocha huyo
Mhispania alitua Goodison Park mwaka 2013, akitokea kufanya kazi Swansea City
na Wigan Athletic. Ni kocha wanne kufundisha muda mrefu katika Premier League
kati ya makocha wa sasa baada ya Arsene Wenger, Eddie Howe na Mark Hughes.
Martinez mwenye miaka 42, ametimuliwa huku akiwa bado na miaka mitatu katika
mkataba wake aliosaini kiangazi cha mwaka 2014.
0 comments:
Post a Comment