Friday 13 May 2016

MAJERUHI :: WELBECK KUIKOSA MICHUANO YA EURO


Image result for DANNY Welbeck injured

DANNY Welbeck atakosa fainali za Euro 2016 baada ya vipimo vya awali kuonyesha kuwa huenda akawa nje ya uwanja kwa miezi mitano. Straika huyo wa Arsenal alipata majeraha ya goti wakati wa ipindi cha kwanza cha mechi yao ya Jumapili waliyotoka sare ya 2-2 dhidi ya Manchester City baada ya kugongana na Bacary Sagna.
Image result for DANNY Welbeck injured

 Welbeck alifahamu haraka kwamba tatizo hilo ni kubwa kutokana na uzoefu alioupata katika majeraha mengine tofauti ya goti yaliyomuweka nje ya uwanja kwa miezi 10. Vipimo vya awali vimeonyesha kuwa straika hyo, 25, atakosa kuitumikia timu ya taifa ya England katika Euro 2016 na huenda akakosekana pia katika mwanzo wa msimu ujao wa Arsenal. 

Nyota huyo wa zamani wa Manchester United alifunga magoli matano na kutoa “asisti” mbili wakati waliporejea bada ya kusubiriwa sana Februari na kuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Arsenal Wenger katika siku za mwisho za msimu. 

Uthibitisho wa ukubwa wa tatizo ulitarajiwa kutolewa jana, lakini vipimo vya awali vinaonyesha kwamba Welbeck, pamoja na majeruhi Alex Oxlade Chamberlain, hawatashiriki fainali hizo za mataifa ya Ulaya nchini Ufaransa Juni, mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA