TBL GROUP YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA WA TUZO YA MZALISHAJI BORA WA MWAKA 2015
Kampuni ya TBL
Group imeibuka mshindi wa kwanza wa tuzo ya Rais ya mzalishaji bora kwa kipindi
cha mwaka 2015,vilevile imeibuka mshindi wa kwanza katika kundi la uzalishaji
wa vinywaji ambapo imetunukiwa tuzo kwa ushindi huo.
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group na maofisa waandamizi wa kampuni wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo
Rais John Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na watendaji wa makampuni ambayo yameshinda tuzo mbalimbali katika kipindi cha mwaka huu
|
Tuzo ya mzalishaji bora
hutolewa na Chama Cha Wenye Viwanda Tanzania (CTI na hafla ya
kukabidhi tuzo kwa washindi mbalimbali imefanyika leo jijini Dar es salaam
katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo mgeni wa heshima
aliyekabidhi tuzo alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa
John Magufuli.
Akiongea baada ya
hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin,alisema
ushindi huu ni zawadi kwa wafanyakazi wote wa kampuni kwa kuwa
jitihada za kila mmoja ndizo zimepelekea mafanikio haya kupatikana.
“Kwetu TBL Grop tunayo
furaha kwa kushinda tuzo hizi tulizofanikiwa kuzinyakua siku ya leo,haya kwetu
ni mafanikio makubwa na tumefurahi kuona mchango wa uwekezaji wetu unatambuliwa
na tunaendelea kuwa washindi wa tuzo mbalimbali zinazotolewa na taasisi mbalimbali”.Alisema
Jarrin.
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin (wa nne mstari wa mbele kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa kampuni hiyo waliohudhuria hafla ya kukabidhiwa tuzo
|
Alisema TBL Group
itaendelea kufanya uwekezaji zaidi nchini na kuchangia kukua kwa uchumi wa
taifa ikiwemo kuunga mkono jitihada za serikali za kupunguza tatizo la ajira
nchini ambapo mbali na kutoa ajira kwenye viwanda vyake na mtandao wa
wafanyabiashara inaoshirikiana nao tayari imeanzisha miradi ya kuwasaidia
wakulima ambayo tayari imeanza kuonyesha mafanikio kwa kubadilisha maisha ya
wakulima kuwa bora.
“Tunaishukuru serikali ya
Tanzania kwa kufanya kazi kwa karibu na wawekezaji na nina imani tutaendelea
kushirikiana ili kuweza kupata mafanikio zaidi katika siku za usoni”.Alisema.
0 comments:
Post a Comment