WATU MASHUHURI WAHUDHURIA MAZISHI YA BONDIA MUHAMMED ALI :CHEKI PICHA
Bondia bora kuliko wote duniani na mwanaharakati wa haki za binadamu Muhammed Ali amezikiwa jana katika maziko ya binafsi yaliyohudhuriwa na marafiki na familia.
Awali kabla ya maziko hayo maelfu ya mashabiki wa bondia huyo walipata fursa ya kukaa kando ya barabara katika mji aliozaliwa wa Louisville, huko Kentucky na kutoa heshima za mwisho wakati gari lililobeba mwili wake likipita mitani.
Tukio hilo lilifuatiwa na hafla ya kumbukumbu ya Muhammed Ali ambapo watu mashuhuri kadhaa walipata fursa ya kumuelezea Ali, kwa namna mbalimbali walivyomfahamu katika maisha yake.
Waongeaji wa madhehebu ya Kiislam, Kikristo na Wayahudi pamoja na wengineo walimuongelea namna alivyokuwa akipigani haki, huku ujumbea wa rais Barack Obama ukimsifiwa kwa kujiamini.
Aliyekuwa rais wa Marekani Bill Clinton akisoma wasifu wa Muhammed Ali
Mike Tyson, Lenox Lewis na Will Smith wakwanza kulia walikuwa miongoni mwa waliobeba jeneza la Muhammed Ali
Aliyekuwa rais wa Pakistan Hamid Karzai alikuwa ni miongoni mwa waliohudhuria
Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Uingereza David Beckham ni miongoni waliohudhurisha maziko ya Muhammed Ali
0 comments:
Post a Comment