Saturday, 18 June 2016

EURO 2016::MORATA AZIDI KUWA TISHIO APIGA 2 HISPANIA IKISHINDA 3 : 0



Juventus striker Morata takes a strike on goal early in the first half as Turkey No 6 Hakan Calhanoglu looks on in the first half
Morata akipiga mpira uliojaa wavuni kuindikia Hispania bao 
Mabingwa mara mbili wa kombe la Euro timu ya Hispania wamesonga mbele hatua ya 16 bora, kwa kusakata kabumbu safi dhidi ya wachovu Uturuki katika mchezo ulioishia kwa ushindi wa magoli 3-0, huko Nice, Ufaransa.

Kwa rekodi za michuano hiyo ya Euro 2016, Hispania imekuwa timu ya kwanza kufunga magoli zaidi ya mara mbili. Katika mchezo huo Alvaro Morata aliipatia Hispania goli la kwanza na Nalito kuongeza la pili kisha Morata kumalizia la tatu.


Mshambuliaji wa Hispania, Alvaro Morata akishangilia baada ya kuifungia timu yake mabao mawili katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Uturuki usiku wa jana Uwanja wa Allianz Riviera mjini Nice, Ufaransa katika mchezo wa Kundi D Euro 2016.

Kufuatia ushindi huo ni wazi kuwa  Hispania imesonga katika hatua ya 16 bora kwa kufikisha jumla ya alama 6 huku Uturuki ikiwa imeaga michuano hii kwa kuwa na point 0 na sasa wawili hawa wanasubiri mchezo wa mwisho ili kukamilisha ratiba. 
After setting up Morata, Nolito then latched on to a poor defensive header by Topal just two minutes later to make it 2-0
 Bao lingine la mabingwa hao watetezi lilifungwa na Nolito  




0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA