Saturday, 18 June 2016

EURO 2016::ROMELU LUKAKU APIGA MBILI UBELGIJI IKIPATA USHINDI WAKE WA KWANZA


Mshambuliaji Romelu Lukaku amefumania nyavu mara mbili wakati Ubelgiji ikipata ushindi wake wa kwanza katika michuano ya Euro 2016 na kuichakaza Jamhuri ya Ireland kwa magoli 3-0.

Baada ya kipindi cha kwanza kuisha bila ya kupatikana goli, Romelu Lukaku, alifunga goli lake la kwanza katika michuano hiyo kwa kutumbukiza mpira pembeni mwa goli la Jamhuri ya Ireland.
Mchezaji Axel Witsel alifunga goli la pili la Ubelgiji kwa kichwa katika dakika ya 61, kabla ya Romelu Lukaku tena kuachia shuti lililojaa wavuni kufuatia kufanywa shambulizi la kushtukiza.
                           Romelu Lukaku akiachia shuti lililozaa goli la tatu kwa Ubelgiji
                                 Axel Witsel akishangilia goli lake alilofungwa kwa kichwa 
Romelu Lukaku akitokwa na machozi baada ya kufunga goli la kwanza akiwa anashagilia na mdogo wake Jordan

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA