MTU MWENYE SILAHA AUWA WATU 50,AJERUHI WENGINE 53 KWENYE KLABU YA MASHOGA MAREKANI
Watu 50 wamethibitishwa kufa katika tukio la shambulizi la silaha kwenye klabu ya usiku ya mashoga huko Orlando, Florida, huku hali ya tahadhari ikitangazwa kwenye mji huo na Meya Buddy Dyer.
Mtu huyo aliyekuwa na silaha ametambulika kama Omar Mateen, naye aliuwawa baada ya kuwashikilia watu mateka. Watu wengine 53 wamejeruhiwa kwenye tukio hilo katika klabu ya Pulse.
Tukio hilo la shambulizi la kutumia silaha ni baya kuwahi kutokea katika historia ya Marekani, ambapo tayari polisi wamesema ni tukio la kigaidi lililotokana na misukumo ya kiimani.
Akilihutubia taifa Rais wa Marekani , Obama alisema shambulio hilo ni ishara ya ugaidi na chuki huku akisisitiza kuwa siyo tu kwa jamii ya mashoga bali ni kwa jamii nzima ya Marekani.
Polisi akiwa amevalia nguo za kazi katika eneo la tukio la kigaidi huko Orlando, Florida Marekani
Mshambuliaji aliyeuwawa Omar Mateen akiwa amepozi akijipiga picha za Selfie kwa kutumia simu na kioo.
Sambamba na hilo mgombea anewania kuteuliwa na chama chake kuwania Urais Donald Trump amezidi kupigilia msumari msimamo wake juu ya waislamu wenye itkadi kali na aliandika haya katika mtandao wa kijamii wa twiter.
Watu waliopatwa na mshtuko baada ya kutokea tukio hilo la shambulizi la kutumia risasi katika klabu ya Pulse.
0 comments:
Post a Comment