SERENGETI BOYS YAINGIA KAMBINI KUJINOA DHIDI YA SHELI SHELI
Na Mwandishi Wetu
TIMU ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 'Serengeti Boys' imeingia kambini leo Jumanne, kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Shelisheli mchezo utakaochezwa Juni 26 katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Serengeti Boys ambayo ipo chini ya kocha Bakari Shime itacheza mechi ya marudiano na Shelisheli, Julai 2 huko Shelisheli.


Kikosi ambacho kimeingia kambini kinaundwa na makipa Kelvin Deogratius Kayego,
Ramadhani Awm Kambwili na Samwel Edward Brazio.
Mebeki ni Kibwana Ally Shomari, Israel Patrick Mwenda, Anton Shilole Makunga, Nickson Clement Kibabage, Dickson Nickson Job, Ally Hussein Msengi na Issa Abdi Makamba.
Viungo ni Kelvin Nashon Naftal, Ally Hamis Ng’anzi, Shaban Zuberi Ally, Mustapha Yusuph Mwendo, Yassin Muhidini Mohammed, Syprian Benedictor Mtesigwa, Gadafi Ramadhan Sai, Asad Ali Juma, Mohammed Abdallah Rashid na Muhsin Malima Makame.
Washambuliaji ni Ibrahim Abdallah Ali, Enrick Vitaris Nkosi, Rashid Mohammed Chambo na Yohana Oscar Mkomola.
Katika kujindaa na mchezo huo, Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako walishiriki mashindano ya vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF International Youth Tournament 2016) .
0 comments:
Post a Comment