 |
Giroud akiifungia Ufaransa kwa guu la kushoto dakika ya 12 |
Wenyeji wa michuano ya Euro 2016 -
Ufaransa wametinga hatua ya nusu fainali kwa kishindo baada ya kuitandika
Iceland 5-2 katika mchezo uliopigwa usiku wa kuamkia leo.
 |
Pogba akijitwisha kichwa kilichozaa bao la pili |
 |
DAB:: Pogba akishangilia kwa staili maarufu kwa jina la Dab |
Iceland iliyoing'oa England katika hatua ya mtoano, ilishindwa
kabisa kufurukuta na kujikuta ikienda mapumziko ikiwa nyuma kwa bao 4-0 kwa
magoli yalifungwa na Olivier Giroud, Paul Pogba, Dimitri Payet na Antoine
Griezmann katika dakika ya 12, 19, 43 na 45.
 |
Winga mahiri wa klabu ya WestHam United ambaye amekuwa moto wa kuotea mbali katika michuano hii akipachika bao la tatu kwa Ufaransa
|
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo Iceland walifanikiwa kupata
bao kupitia kwa Kolbeinn Sigthorsson kunako dakika ya 56 kabla Olivier Giroud
hajaifungia Ufaransa bao la tano dakika ya 56 huku Birkir Bjarnason akiipa bao la pili Iceland
dakika ya 84.
 |
Kiungo wa Iceland Birkir Bjarnason akiindikia bao la pili timu yake katika dakika za lala salama |
0 comments:
Post a Comment