Monday, 22 August 2016

SERENGETI BOYS YAZIDI KUIKARIBIA MICHUANO YA AFRIKA 2017

Timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya vijana wenzao wa Afrika Kusini ‘Amajimbo’ katika mchezo wa marudiano ya kufuzu kwa mashindano ya Mataifa ya Afrika.

Katika mchezo wa awali, Serengeti Boys ilifanikiwa kulazimisha sare ya ugenini na kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele.

Vijana hao wa kocha Bakari Shime, walianza mchezo kwa kasi wakihitaji ushindi wa nyumbani ili kujisogeza katika hatua inayofuata.

Mabao ya Serengeti Boys yalifungwa na Mohammed Abdallah dakika ya 34 na la pili lilipachikwa nyavuni na Muhsin Makame na kuihakikishia Serengeti Boys nafasi ya kusonga mbele katika michuano hiyo kwa ushindi wa mabao 2-0.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA