Sunday 18 September 2016

WATFORD WAIBATIZA MANCHESTER UNITED MARA TATU

Timu ya Manchester United imejikuta ikipata kipigo cha tatu mfululizo baada ya kufundishwa soka na Watford na kukubali kipigo cha magoli 3-1 katika dimba la Vicarage Road.

Baada ya kupoteza mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Manchester City, na kisha baadaye wa Ligi ya Uropa dhidi ya Feyenoord, kikosi cha Jose Mourinho kimepata kipigo tena hii leo.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Uingereza, Etienne Capoue, aliifungia Watford goli la kwanza kabla ya Marcus Rashford kusawazisha.

Hata hivyo, Juan Camilo Zuniga akitokea benchi alifunga goli la pili baada ya kuugusa mpira kwa mara ya kwanza na kisha Troy Deeney akifunga la tatu kwa mkwaju wa penati.
                                                Etienne Capoue akiifungia Watford goli la kwanza 
Martial tries to find a path past Watford midfielder Valon Behrami during the first-half

                               Marcus Rashford akifunga goli pekee la Manchester United


United manager Jose Mourinho looks anxious on the bench as they fall behind during the first period
Kocha Jose Mourinho akiwa haamini kinachotokea

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA