Sunday 9 October 2016

STURRIDGE, DELE ALI WAIBEBA UINGEREZA IKIIBUKA NA USHINDI DHIDI YA TIMU YA TAIFA YA MALTA

Kocha Gareth Southgate amepata ushindi wake wa kwanza akiiongoza timu ya taifa ya Uingereza baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya timu ya taifa dogo la Malta.

Katika mchezo huo wa kuwania kufuzu kutinga michuano ya kombe la dunia 2018 Daniel Sturridge na Dele Alli walifumania nyavu, na kuifanya Uingereza kuongoza kundi F kwa pointi 6.

Katika mchezo huo kapteni Wayne Rooney ameendelea kutoonyesha kiwango kizuri na kupelekea kuzomewa na mashabiki wa Uingereza, licha ya kutetewa mno na kocha Gareth Southgate.
       Daniel Sturridge akipiga mpira wa kichwa uliojaa wavuni na kuandika goli la kwanza
                             Dele Alli akidokoa mpira kwa mguu na kufunga goli la pili la Uingereza
 Jesse Lingard akizuiliwa na kipa wa Malta asifunge goli katika mchezo wake wa kwanza akiwa na timu ya taifa

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA