Sunday 2 October 2016

TOTTENHAM YAVURUGA RAHA NA REKODI YA MANCHESTER CITY KUTOFUNGWA


Tottenham imemaliza rekodi ya kuanza vyema Ligi Kuu ya Uingereza kocha Pep Guardiola, kwa kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Manchester City katika dimba la White Hart Lane.

Guardiola alikuwa ameshinda michezo yake sita ya awali, lakini katika mchezo wa leo City ilijikuta ikizidiwa kila idara na Tottenham ambao sasa wamebakia kuwa timu pekee ambayo haijafungwa katika Ligi Kuu ya Uingereza.

Spurs walitawala mchezo huo tangu mwanzo ambapo walipata goli lao la kwanza katika dakika ya tisa baada ya Aleksandar Kolarov kujifunga katika harakati za kuokoa krosi iliyopigwa na Danny Rose, huku Dele Alli akifunga goli pili.
                     Beki wa Manchester City Aleksandar Kolarov akiwa anajutia goli la kujifunga
      Dele Alli akiangalia shuti lake alilopiga likimshinda kipa na kuiandikia Tottenham goli la pili

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA