Saturday 1 October 2016

WANATISHA::LIVERPOOL YATOKA NYUMA NA KUIBUKA NA USHINDI DHIDI YA SWANSEA

Penati ya dakika za mwisho ya James Milner imeipatia Liverpool ushindi waliopigania mno wa magoli 2-1 kutoka kwa Swansea, na kuongeza machungu kwa kibarua cha kocha wa Swansea Francesco Guidolin.

Katika mchezo huo Leroy Fer alikuwa wa kwanza kutikisa nyavu za Liverpool na kuwafanya wenyeji kuongoza kwa goli alilofunga kwa karibu akiugonga mpira uliogonga mwamba baada ya kupigwa na Baston Borja.

Mshambuliaji Roberto Firmino aliisawazishia Liverpool dakika chache baada ya mapumziko akiunganisha krosi ya Jordan Henderson, na kisha baadaye Milner akafunga goli la ushindi dakika sita kabla ya mchezo kumalizika.
                                           Leroy Fer akifunga goli la kwanza katika mchezo huo
            Mpira wa kichwa uliopigwa na Roberto Firmino ukimzidi kipa na kutinga wavuni

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA