UEFA::LEICESTER CITY YAFUZU HATUA YA ROBO FAINALI
Leicester City imeandika ukurasa mwingine katika historia ya soka klabuni hapo baada ya kubadili matokeo ya kufungwa katika mchezo wa kwanza kwa kufanikiwa kuifunga Sevilla magoli 2-0 na kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Leicester ilionekana kama itatolewa baada ya kufungwa magoli 2-1 Hispania katika mchezo wa kwanza na kutimuliwa kocha wao Claudio Ranieri, ambaye aliiongoza hadi kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza kwa mara ya kwanza.
Ikiwa chini ya kocha wa muda Craig Shakespeare, Leicester imebadilika na ilikuwa katika kiwango kizuri jana ambapo nahodha wao Wes Morgan aliipatia goli la kwanza katika kipindi cha kwanza na kisha baadaye Marc Albrighton kufunga la pili.
Beki Wes Brown akifunga goli la kwanza la Leicester City
Marc Albrighton akifunga goli la pili na kuizamisha Sevilla
0 comments:
Post a Comment