WANANCHI WA MKOA WA ARUSHA WAJITOKEZA KWA KASI KUPATA HUDUMA YA KUPIMA AFYA ZAO BURE KATIKA WIKI YA WANAWAKE DUNIANI
Baadhi ya wananchi wakichukuliwa vipimo vya afya na madaktari kutoka kcmc pamoja na Mounti meru Hospital ikiwa ni huduma inayotolewa bure katika viwanja vya kumbukumbu ya sheikh Amri Abeid katika wiki ya wanawake duniani ambayo kwa mkoa wa Arusha imeandaliwa na Phide intantament
Baadhi ya wananchi wakiwa katika mstari wakisubiri kuchukuliwa vipimo vya magonjwa mbalimbali bure yakiwemo ,Kisukari ,Presha,Kansa ,Ukimwi na mengineyo
Mmoja wa madaktari akiendelea kupima mara baada ya kuchukuwa vipimo vya wagonjwa ndani viwanja vya Sheikh Amri Abeid Na Woinde Shizza,Arusha
Maadhimisho ya wiki ya wanawake duniani yameanza rasmi mkoani Arusha ambapo wananchi wa mkoa wa Arusha pamoja na vitongoji vyake wamepata fursa ya kupata huduma ya kupima magonjwa mbalimbali bure
zoezi hilo ambalo limeanza leo jijini hapa katika kiwanja cha sheikh Amri Abeid limeonekana kuwavuta wananchi wengi kwani zaidi ya wananchi 100 wamejotokeza kupima afya zao bure katika viwanja hivyo
Akiongea na waandishi wa habari muandaaji wa maathimisho hayo ya wiki ya wananwake duniani kwa mkoa wa Arusha mkurugenzi wa Phide Intantament Phidesia Mwakitalima alisem akuwa muamko ni mzuri na wananchi wameanza kujitokeza kwa wingi
Alisema kuwa pamoja ni siku ya kwanza tu lakini zaidi ya wananchi 100 wamejitokeza kupima afya zao hivyo ni jambo zuri mno
Alisema kumekuwepo na tabia ya wananchi wengi kutokuwa na tabia ya kupima afya zao hadi pale wanapoumwa kitu ambacho sio kizuri na kuwataka wananchi kujijengea tabia ya kupima afya zao mara kwa mara Zoezi hili la kupima afya limeanza leo na linatarajiwa kumalizika march nane na huduma za kupima magonjwa mbalimbali na ushauri wa aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na watu kuchangia damu unatolew bure hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kutumia fursa hiii ili kujua afya yake.
0 comments:
Post a Comment