SIKU YA WANAWAKE DUNIANI, TUTCA YAENDESHA KONGAMANO LENGO KUPAZA SAUTI JUU YA UNYANYASAJI WA KIJINSIA KATIKA MAENEO YA KAZI
Mgeni Rasmi katika Kongamano la Siku ya wanawake Duniani katika Kupaza sauti juu ya unyanyasasaji wa kijinsia katika maeneo ya kazi Mh. Magreth Sitta (MB) akitoa hotuba yake na kufungua rasmi mjadala
Mkurugenzi wa Jinsia na Vijana TUCTA Bi.Siham Ahmed akizungumza katika Kongamano hilo na kusema kuwa lengo kubwa ni kupanua wigo wa kuwapigania wanawake kwani ukatili huo upo kuanzia ngazi ya familia.
Mwenyekiti wa wanawake Rehema Ludaga akitoa utambulisho kwa viongozi mbalimbali waliofika katika Kongamano hilo
Katibu Mkuu wa TUCTA Dkt. Msigwa akitoa nasaha zake wakati wa kongamano hilo
Rais wa TUCTA Bw. Gratian Mkoba akizungumza na wakina mama pamoja na wadau mbalimbali katika Kongamano hilo.
Mmoja wa washiriki katika Kongamano hilo akitoa salamu za shukurani kwa Mgeni Rasmi wakati wa Kongamano hilo
Baadhi ya wajumbe wakiwa katika Kongamano hilo
Picha zote na Fredy Njeje wa Blogs za Mikoa
Story na Dickson Mulashani- Funguka Live Blog
Katika
maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani,
Chama Cha Wafanyakazi nchini (TUCTA) kimeendesha
kongamano la wanawake nchini kupitia uwakilishi wa vyama vyao lenye lengo la
kupaza sauti juu ya ukatili wa kijinsia hasa unyanyasaji wa wanawake katika
maeneo ya kazi ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mh Mbunge wa Bunge la Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania mama Magreth Sitta.
Katika kongamano hilo lililohudhuriwa na wawakilishi wa vyama vya wafanyakazi vikiwemo
RAAWU, TUGHE,TALGWU,TASU, CWT ,TEWUTA,DOWUTA, TRAWU, CHODAWU,TUICO na COTWU(T) lililodhaminiwa na SSRA, shirika la kazi
duniani ILO kampuni ya Mo Dewji Foundation pamoja na Global Peace Fodation ambao ndio walioshiriki kufanikisha kongamano hilo lil0beba
kauli mbiu isemayo “Kukomesha na Kuzuia Ukatili na Unyanyasaji Dhidi ya Wanawake Mahala pa Kazi” likilenga ikilenga kutanua wigo wa kuwapigania wanawake kwani
vita hii ilielemea zaidi katika ngazi za kijamii na hasa familia.
Akizungumza wakati wa ufunguzi, Rais wa chama cha
wafanyakazi TUCTA Ndg.Gratian Mukoba amepongeza jitihada zinazofanywa na
wanawake katika maeneo waliopo na kuwasihi washikamane na kudumisha upendo
baina yao ili kuujenga ukuta imara dhidi ya manyanyaso dhidi yao na kuwaomba
wazingatie suala la afya katika maeneo yao ya kazi . “Bila kuwa na afya bora
mapambano haya hayatakuwa na tija, ni muhimu kuhakikisha hata maeneo yetu ya
kazi yanakuwa na vyoo vya kutosha na vyenye kukidhi mahitaji ya kijinsia ,haipendezi
watu wa jinsia moja kushiriki katika maliwato moja na endapo kuna ” alisema
Ndg. Mukoba.
Aidha kongamano hilo limebainisha miongoni mwa
manyanyaso wanayopata wanawake katika maeneo ya kazi ni pamoja na kiakili na
kimwili kutokana na vitendo kama kutopandishwa vyeo,kunyima ruhusa za kwenda
masomoni,kupewa uhamisho usio na tija manyanyaso vya kingono ikiwemo hata
wakati wa kuomba ajira.
Alipokaribishwa kufungua rasmi kongamano hilo, Mgeni
rasmi Mh.Magreth Sitta alijikita kuwahimiza wanawake kujitoa na kugombea katika
nafasi mbalimbali katika nyadhifa tofauti ambazo zipo katika maeneo yao ya kazi
na maadam wanakidhi vigezo huku akitumia historia yake ya uongozi kama ushuhuda
na hamasa kwao.
Sambamba na hilo amewataka akina mama kupitia vyama
vyao kuhakikisha wanaweka mikakati makini ili kuweza kushabihiana na malengo ya
serikali na kujiweka katika mfumo wa kuchangia kuijenga Tanzania ya Viwanda
huku akigusia kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kitaifa.
Kongamano
hili lilianza kufanyika mnamo miaka ya tisini na huadhimishwa kila mwaka siku
moja kabla ya tarehe ya kilele ya siku ya wanawake duniani.
0 comments:
Post a Comment