STARS YAVUNJA MWIKO DHIDI YA BAFANA BAFANA NA KUTINGA NUSU FAINALI COSAFA CUP
Mshambuliaji timu ya taifa ya Tanzania na shujaa wa mchezo huo Elias Maguri akipambana na Beki wa Bafana Bafana Nurdin katika mchezo uliomalizika kwa ushindi wa goli moja kwa bila kwa Taifa Stars Picha na Mtandao |
Taifa Stars imetinga nusu fainali ya michuano ya Cosafa baada ya kuwatwanga wenyeji Afrika Kusini kwa bao 1-0.
Shuja wa mechi hiyo ambaye pia ameibuka nyota wa mchezo huo amekuwa ni Elius Maguri ambaye amefunga bao hilo pekee katika kipindi cha kwanza.
Kipa Aishi Manula mara kadhaa alilazimika kuokoa michomo mikali ya washambuliaji wa Afrika Kusini.
Safu ya ulinzi iliyoongozwa na Erasto Nyoni na Salim Mbonde ilionekana kukaa imara tokea kipindi cha kwanza lakini Muzamiru Yassin na Raphael Alpha wakaonekana kufanya vizuri zaidi katika kuisadia timu wakitokea eneo la kati la uwanja huku Simon Msuva aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Thomas Ulimwengu na kusaidia kuongeza nguvu ya kupandisha presha kwenye lango la Afrika Kusini.
Sasa Taifa Stars itaumana na Zambia katika mchezo wa nusu fainali siku ya Jumatano tarehe 5 Julai.
0 comments:
Post a Comment