NEC YATEUWA MADIWANI 12 WANAWAKE WA VITI MAALUM
Kwa Mujibu wa Kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika kikao chake cha kawaida kilichofanyika tarehe 21 Agosti, 2017 na baada ya kushauriana na Vyama vya Siasa imewateua Madiwani Wanawake wa Viti Maalum kumi na wawili (12) kujaza nafasi wazi za Madiwani katika Halmashauri mbalimbali Tanzania Bara.
Madiwani Wanawake wa Viti Maalumu walioteuliwa ni kama ifuatavyo:
NA. | JINA | CHAMA | HALMASHAURI |
| Ndugu Saida Idrisa Kiliula | CUF | Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa |
Ndugu Sophia Charokiwa Msangi | CCM | Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga | |
Ndugu Shahara Selemani Nduvaruva | CCM | Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali | |
Ndugu Neema K. Nyangalilo | CCM | Halmashauri ya Manispaa ya Ilala | |
Ndugu Farida Zaharani Mohamed | CCM | Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero | |
Ndugu Lucia Silanda Kadimu | CCM | Halmashauri ya Wilaya ya Tabora (Uyui) | |
Ndugu Amina Ramshi Mbaira | CCM | Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu | |
Ndugu Janeth John Kaaya | CHADEMA | Halmashauri ya Wilaya ya Meru | |
Ndugu Sara Abdallah Katanga | CHADEMA | Halmashauri ya Manispaa ya Ilala | |
Ndugu Ikunda Massawe | CHADEMA | Halmashauri ya Wilaya ya Hai | |
Ndugu Tumaini Wilson Masaki | CHADEMA | Halmashauri ya Wilaya ya Siha | |
Ndugu Elizaberth Andrea Bayyo | CHADEMA | Halmashauri ya Mji wa Mbulu |
Uteuzi huu umefanyika baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa ambaye kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 alitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi uwepo wa nafasi hizo wazi.
Imetolewa tarehe 21 Agosti, 2017
Kailima, R. K
MKURUGENZI WA UCHAGUZI
0 comments:
Post a Comment