Showing posts with label uchaguzi. Show all posts
Showing posts with label uchaguzi. Show all posts

Tuesday, 26 September 2017

RUTAINURWA ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI MPYA JUMUIA YA WAZAZI WILAYA YA ILALA



NA BASHIR NKOROMO
Lucas Rutainurwa ametawazwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi wa Jumuiya hiyo uliofanyika jana.

Katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Lugano Mwafongo, amesema katika Uchaguzi huo uliofanyika Segerea, Rutainurwa (pichani), alipata kura 278 dhidi ya Mohamed Honelo aliyepata kura 148 baada ya hao wawili kuingia katika kinyang'anyiro kwa mara ya pili kufuatia kutopatikana mshindi aliyepata zaidi ya nusu ya kura zilizopigwa  katika uchaguzi wa awali.

Wakati katika awamu ya kwanza  Lutainurwa alipata kura 277 Honelo alipata kura 243 huku Celestine Nyalusi akipata kura 67.

Nafasi ya Mjumbe wa Halimashauri Kuu aliyeshinda ni George MJtambalike ambaye amepata kura 195 dhidi ya Edward Haule aliyepata kura 181. PICHA ZA UCHAGUZI HUO/>BOFYA HAPA

Friday, 1 September 2017

BREAKING NEWS: MAHAKAMA KUU YA KENYA YAAMURU UCHAGUZI MKUU WA KENYA URUDIWE BAADA YA SIKU 60

Image result for uchaguzi kenya 2017


Image result for uchaguzi kenya 2017




















MAHAKAMA Kuu nchini Kenya, imetengua ushindi wa Rais wa sasa Uhuru Kenyatta, dhidi ya hasimu wake mkuu Raila Odinga, urudiwe ndani ya siku 60 kuanzia leo Septemba 1, 2017.

Mahakama Kuu ya Kenya, imefikia uamuzi huo leo Septemba 1, 2017, kufiuatia maombi ya Mgombea wa Muungano wa upinzani NASA, chini ya mgombea wake, Bw. Raila Odinga, ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais uliofanyika Agosti 8, 2017 na kumpa ushindi Rais Kenyatta.

Katika maombi yake, Bw. Odinga alisema, kura zake zilipunguzwa kwenye baadhi ya vituo na kuongezewa kwa mpinzani wake, lakini kubwa zaidi ni kukiukwa kwa taratibu za uchaguzi ambapo baadhi ya fomu muhimu za matokeo ya uchaguzi kama vile fomu namba 34A,B na C, hazikupatikana siku ya kutangazwa kwa matokeo.


Katika uamuzi wa mahakama hiyo, majaji wanne kati ya sita (6), wamekubaliana kuwa tume huru ya uchaguzi na mipaka ya Kenya, (IEBC), imeshindwa kusimamia vema uchaguzi huo na hivyo kusababisha kasoro kadhaa ambazo zinakwenda kinyume na katiba ya Kenya. Hata hivyo, Mahakama hiyo imesema, hakuna ushahidi wowote, ulioonyesha kuwa Rais Uhuru Kenyatta, alitenda makosa katika mchakato huo wa uchaguzi.

Tuesday, 22 August 2017

NEC YATEUWA MADIWANI 12 WANAWAKE WA VITI MAALUM

Kwa Mujibu wa Kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika kikao chake cha kawaida kilichofanyika  tarehe 21 Agosti, 2017 na baada ya kushauriana na Vyama vya Siasa imewateua Madiwani Wanawake wa Viti Maalum kumi na wawili (12) kujaza nafasi wazi za Madiwani katika Halmashauri mbalimbali Tanzania Bara.
 
Madiwani Wanawake wa Viti Maalumu walioteuliwa ni kama ifuatavyo:

NA.JINACHAMAHALMASHAURI
  1. 1
Ndugu Saida Idrisa KiliulaCUFHalmashauri ya Wilaya ya Kilwa

Ndugu Sophia Charokiwa MsangiCCMHalmashauri ya Wilaya ya Mwanga

Ndugu Shahara Selemani NduvaruvaCCMHalmashauri ya Wilaya ya Mbarali

Ndugu Neema K. NyangaliloCCMHalmashauri ya Manispaa ya Ilala

Ndugu Farida Zaharani MohamedCCMHalmashauri ya Wilaya ya Mvomero

Ndugu Lucia Silanda KadimuCCMHalmashauri ya Wilaya ya Tabora (Uyui)

Ndugu Amina Ramshi MbairaCCMHalmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

Ndugu Janeth John KaayaCHADEMAHalmashauri ya Wilaya ya Meru

Ndugu Sara Abdallah KatangaCHADEMAHalmashauri ya Manispaa ya Ilala

Ndugu Ikunda MassaweCHADEMAHalmashauri ya Wilaya ya Hai

Ndugu Tumaini Wilson MasakiCHADEMAHalmashauri ya Wilaya ya Siha

Ndugu Elizaberth Andrea BayyoCHADEMAHalmashauri ya Mji wa Mbulu

Uteuzi huu umefanyika baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa ambaye kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 alitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi uwepo wa nafasi hizo wazi.
 
Imetolewa  tarehe 21 Agosti, 2017
Kailima, R. K
 
MKURUGENZI WA UCHAGUZI

Saturday, 12 August 2017

RAIS MAGUFULI AMPONGEZA UHURU KENYATTA KWA USHINDI KENYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 12 Agosti, 2017 amempongeza Rais Mteule wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta baada ya jana kutangazwa mshindi wa nafasi ya Urais na Tume Huru Ya Uchaguzi Kenya ( IEBC).

Tume Huru ya Uchaguzi Kenya ilitangaza Kenyatta kuwa mshindi kwa kupata kura 8,203,290 (54.27%) dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga 6,762,224 (44.74%), kufuatia matokeo hayo Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ametoa pongezi kwa Uhuru Kenyatta kwa kuchaguliwa kwa mara nyingine tena.

"Nakupongeza Ndg.Uhuru Kenyatta kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Kenya kwa kipindi kingine. Nakutakia mafanikio mema" alisema Rais Magufuli kupitia mtandao wake wa Twitter

Kwa mujibu wa Tume Huru ya Uchaguzi Kenya (IEBC) ilisema kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa huru na haki na kudai kuwa umekuwa ni uchaguzi wa kipekee kwa Kenya kwani watu waliojitokeza kujiandikisha na kupiga kura ni wengi zaidi ukilinganisha na chaguzi zilizofanyika kipindi cha nyuma.

UHURU KENYATTA ATANGAZWA MSHINDI WA URAIS KENYA

Tume huru ya uchaguzi Kenya (IEBC) imemtangaza Uhuru Kenyatta kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Jumanne akipata kura 8,203,290.

Mwenyekiti wa tume hiyo, Wafula Chebukati amekabidhi cheti cha ushindi kwa Kenyatta na mgombea mwenza wake William Ruto.

Akihutubia jana mara baada yakutangazwa kuwa mshindi, Rais Kenyatta amewashukuru wananchi kwa kuwa na imani naye na serikali yake.

“Nawaahidi tutaendelea na kazi tuliyoianza. Nawashukuru sana Kenya. Kadhalika, naishukuru tume ya uchaguzi kwa kazi nzuri waliyoifanya,” alisema.

“Nawapongeza wote walioshinda, na kwa walioshindwa pia tutaishi kupambana siku nyingine.”

Kwa upinzani alisema: “Sisi si maadui, ni raia wa nchi moja. Kila shindano, kutakuwa na washindi na wanaoshindwa, lakini tutasalia kuwa Wakenya. Nawapa moyo wa ushirikiano, twafaa kuungana pamoja. Wakenya wanataka sisi tufaulu.”

“Sana kwa Raila Odinga, namuomba yeye, wafuasi wake, wote waliochaguliwa kupitia upinzani, tutafanya kazi pamoja, tutashirikiana, tutakua pamoja na kuendeleza nchi pamoja.”

“Kwa Wakenya wenzangu, uchaguzi huja na kuondoka lakini Kenya itaendelea kuwepo, tukumbuke daima kwamba sisi ni ndugu na dada. Jirani yako bado ni jirani yako. Tuendelee kudumisha amani. Hakuna haja ya fujo, sisi wanasiasa pia huja na kuondoka. Lakini jirani yako atabaki.”

Katika takwimu
  • Bw Kenyatta alipata kura 8,203,290 sawa na asilimia 54.27 ya kura zilizopigwa
  • Bw Raila Odinga alipata kura 6,762,224 sawa na asilimia 44.74 ya kura zote zilizopigwa
  • Waliojitokeza walikuwa 15,073,662 ambayo ni asilimia 78.91 kati ya 19m waliokuwa wamejiandikisha kupiga kura
  • Siku ya Alhamisi upinzani ulidai  kwamba Raila Odinga alishinda uchaguzi na kuitaka tume imtangaze kuwa mshindi wa urais

Wednesday, 28 October 2015

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA