Monday 4 September 2023

TUNAPASWA KUWAAMBIA HAYA VIJANA WETU KABLA HAWAJAANZA KUJITEGEMEA



Ukiwa mzazi, au mlezi
 lazima kuna kipindi unapata hofu na mtoto wako. Ambaye unaona anaelekea katika rika la ujana na kepuvuka.

Unafikiria mambo mengi ambayo wewe unayafahamu kama changamoto katika maisha ya ujana ambayo  uliyapitia,na unaona kabisa na yeye sasa anaenda kukumbana nayo.

Hofu yako kubwa ni, hujui atatumia njia gani kukwepa mitego ya jamii na kama ataingia kwenye mtego na kunaswa atatokaje?

Kwani kiuhalisia kijana wako, anapoanza kuchangamana na vijana wengine wenye historia 
mbali mbali huwa katika uwezekano wa kuchota tabia zao kwa kuwa anatumia muda mwingi kuwa nao kuliko wewe.

Ushahidi unaonyesha kuwa vijana wengi ambao walikuwa wanapewa usia wa mambo ya maisha na wazazi wao,walifanikiwa kukwepa mitego hiyo kwa kukumbuka maneno ya mzazi, na hofu kutotaka kwenda kinyume na maelekezo yao.



Kuna kipindi, wewe mzazi, mlezi, Kaka au dada unaona kabisa kijana wako anaonyesha mabadiliko ya tabia,lakini unajisikia aibu kukaa naye chini na kumpa ukweli wa mambo ulivyo.

Kwani waswahili wanasema;"Samaki mkunje angali mbichi"Ukishamkosea katika rika hili,
basi uombe, awe na uzoefu binafsi wa kutambua  vita iliyo mbele yake ni ya namna gani na vipi ataishinda.

Hapa tuangalie mambo 7 ambayo mzazi unapaswa uanze kuzungumza na kijana wako:

1.NGONO NA JINSIA


Kijana wako, ambaye anakua atakutana na taarifa nyingi sana kuhusu ngono na jinsia. Ambazo nyingi sana huko mtaani huwa si sahihi.Iwe kupitia vyombo vya habari au uzoefu atakaokutana nao yeye mwenyewe.

Anza kuzungumza naye kuhusu masuala ya uzazi, mimba za utotoni, na utoaji wa mimbahuku ukijikita katika madhara na namna ya kujikinga navyo.

2.DAWA ZA KULEVYA,NA POMBE

Vijana wanapenda sana kuhudhuria burudani kipindiwakiwa mtaani, shule au hata vyuoni miaka ya mwanzoni.Huko wanakuwa katika hatari ya kutumia vilevi kwa kuwa wanakutana na vijana wenzao wenye historia tofauti tofauti.

Kama usipomnyoosha mapema wewe mwenyewe vijana wenzake watamnyoosha katika njia zao.Kwani wengi wao wanaingia katika mkumbo kwa kuwa, hawakupata taarifa sahihi kutoka kwa wenzao juu ya madhara ya tabia hizo,na pia kukwepa kuonekana mshamba.

3.MATUMIZI YA PESA


Kipindi cha ukuaji mahitaji na matumizi ya kijana yanaongezeka kwa kasi kubwa sana,hata kutunza kidogo anachopata kwake huwa ni tatizo.Kaa na kijana wako umuonyeshe namna ya kutunza kidogo anachopata.Mueleze faida za kutunza pesa zilivyo na zitamsaidiaje katika maisha yake ya kujitegemea.

4.UMUHIMU WA FAMILIA





Mara nyingi, vijana wanapopata nafasi ya kufanya shughuli zao wenyewe,kukaa karibu na familia huwa ni kitu kigumu.
Hata muda anaotumia kukaa na wanafamilia wenzake huwa ni mdogo kuliko anaotumia kukaa na marafiki.
Tumia busara zako kumuungabnisha na wanafamilia wengine ili washirikiane kwa pamoja.

5.MAHUSIANO NA MITOKO


Vijana hawaoni tabu kubadilisha marafiki hata kwa mwezi mara nne na bado akajiona yuko juu kwa kuwa anawabadilisha anavyotaka.Usiruhusu kijana wako akue na misingi isiyostahili, kwani itakuja kumuumiza siku zijazo.

 Nawe hautajivunia utakayokuwa unayasikia na kuona kumhusu yeye.Kaa naye kabla hajaingia huko,na ujaribu kumuongoza njia sahihi.

6.MATUMIZI YA MITANDAO


Katika zama hizi ambazo teknolojia ya mtandao wa intaneti imeenea kila mahali.Vijana siku hizi kama wamewekewa gundi hapo,kinachopaswa ni wewe mzazi kumfundisha mambo yapi yana umuhimu na yapi hayana umuhimu kwake katika mtandao wa intaneti mapema sio mpaka ulimwengu wa nje uje umfundishe akiwa ameshaumia.

7.TAFSIRI YA KUFANIKIWA


Vijana wengi, tuna tafsiri tofauti tofauti juu ya maana halisi ya kufanikiwa katika maisha.
Hapa ndipo tunapoanzia kupoteza dira kwasababu tunayoyahangaikia kwa kudhani ndio yatakuwa mafanikio yanakuja kuwa sio.

Iwe katika michezo, elimu, au jambo lolote ambalo litakuwa linahusisha nguvu na akili zake lazima umpe tafsiri sahihi ya kufanikiwa ni kuwa na nini.

Yafuatayo unaweza ukaanza kuyafanya leo:

*Mpe usalama;

*Muonyesha upendo na kumjali;

*Weka misingi yako ambayo yeye ataifuata kipindi yupo chini yako;

*Muadhibu pale inapobidi;

*Kuwa na muda wa kutosha kukaa naye na kuzungumza naye;

*Fuatilia uhusiano wake na wengine;

*Muonyeshe mfano.

Kd Mula anasema"KILA MZAZI ANAPENDA KUONA MTOTO WAKE AKIWA ANAJIHUSISHA NA MAMBO YA MSINGI KATIKA MAISHA YAKE.

UKIANZA KUMTEGENEZEA MAZINGIRA HAYO TANGU MAPEMA UTAWEZA KUJIVUNIA TABIA YAKE YA KESHO.

ISIJE BAADAYE KIJANA WAKO AKAKULAUMU KWAMBA HUKUMUELEZA NA KWAMBA UMECHANGIA KUHARIBU MAISHA YAKE KWA KUKAA KIMYA".

Nikutakie Siku Njema

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA