UKIZITUMIA KAULI HIZI KUMFARIJI MTU ZITAZIDISHA HUZUNI KWA MUHUSIKA
Haya ni makosa ambayo tunayafanya bila kujua, kwasababu katika muda huo, tunakuwa hatuna njia ya kumfanya aliyeondokewa na mali au mtu ajisikie tuko pamoja naye katika machungu.
Na kwakuwa ni vigumu kwa muhusika kukueleza kwamba nataka kufanyiwa au kuambiwa kitu fulani ndio nitajisikia vizuri, inakubidi utumie ujuzi wako binafsi kutafuta njia ya kumfanya ajisikie vizuri.
Hapo sasa balaa ndio linaanza,kwani mara nyingi maneno tunayochagua kumwambia aliyepotelewa hayamfanyi ajisikie poa bali yanamfanya aanze kutafakari ulikuwa na maana gani.
Na hii inatokana na si wote wana uwezo wa kutafakari kauli zinazotolewa na watu wengine katika mtazamo chanya.
Hebu tuangalie maneno ambayo hupaswi kuyasema kwa muhusika:
1."Shukuru (ameishi/umeishi nacho) miaka mingi"
Unapoongea kauli kama hii inampa picha mtu huyo, kwamba jambo hilo lilipaswa kutokea kwake,na hivyo hapaswi kuhuzunika.Yawezekana kuna ukweli ndani yake, lakini unapoongea mbele ya muhusika haitamfanya ajisikie vizuri.
2."Muda wake ulifika"
Hata kama umekosa la kuongea hii kauli sio kabisa,itamfanya akuone umefurahia tukio hilo.
3."Alikosea/Ulikosea sana ku.... "
Ikiwa tukio lilikuwa la ajali, hata kama liliempata alisababisha usiongee kauli kama hii kwa muhusika,itaonekana kana kwamba alifanya uzembe na alistahili kupatwa na hilo.
4."Kuna sababu ya kila kitu"
Hii kauli kweli ina maana, unapofikiria kwa kina lakini si nzuri kuizungumza kwa mtu aliye kwenye majonzi.
5."Usihofu utampata mwengine tu"
Ikiwa mtu amepoteza mtoto, mume au mke, kauli ya kumwambia kwamba asihuzunike na kuwa atapata mwengine tu,itamfanya aone hukuwahi kuona umuhimu wa aliyeondokewa naye,na ulikuwa unaombea hilo litokee.
Mara nyingi maneno haya yanapotamkwa na muhusika yanakuwa na matumaini zaidi kuliko yanapotamkwa na mtu mwengine wa pembeni.
Ni heri utumie maneno kama:
1."Pole sana kwa yaliyotokea"
2."Natamani ningekuwa na maneno mazuri ya kukueleza ujisikie vizuri"
3."Niko pamoja nawe katika hili"
4."Niko pamoja nawe katika sala"
5."Tulimpenda wote"
6."Ukihitaji msaada, niko hapa kwa ajili yako"
TABIA YA KUWAFARIJI WENZETU WANAPOPATWA
NA MATATIZO,
NI NZURI SANA NA ITAWAFANYA
WAJISIKIE VIZURI.
KWELI YAWEZEKANA UNA TAFSIRI YAKO
MOYONI JUU YA TUKIO
LILILOTOKEA,
LAKINI IWEKE MOYONI UKIONA HAITAMFARIJI MUHUSIKA.
WOTE TUNAWEZA KUWA TUMAINI KWA WENGINE
PALE WANAPOPATWA NA
MATATIZO
KWA KUTUMIA MANENO NA NJIA SAHIHI
KUELEZEA HISIA ZETU PIA.
0 comments:
Post a Comment