Wednesday 26 October 2022

ZITAMBUE ZIFA ZA MTU ALIYEKUA KIHISIA





Habari yako msomaji wangu, nianze kwa kukushukuru sana kwa imani na heshima uliyonipa na unayoendelea kunipa katika kipindi chote cha mwaka huu wa 2017 na tunapoelekea mwishoni, nakutakia kila kheri na Mungu akakupe yale unliyomuomba na pia tukijaaliwa kuuvuka mwaka,2018 ukawe mwaka wa kupiga hatua za kusonga mbele.

Katika miaka ya hivi karibuni suala la rika limekuwa likipoteza uhalisia na sasa mipaka ya umri katika masuala mbali mbali ni kama inapotea hasa kwa vijana.
Vijana wengi wanapoona wamepata urefu, mabadiliko ya mwili, kupanda kielimu, na hata kazi wanajiona tayari wameshakua.


Katika mazingira ya elimu kama chuo na kazini,vijana wengi wamekuwa kitaaluma na kiujuzi, lakini kihisia bado wanakuwa ni wadogo japo wanashindwa kulitambua hilo.

Jibu linaweza kuja kwa haraka kwamba,hiki ni kizazi cha vijana wanaojua vitu vingi mapema kabla ya umri wao.


Kiuhalisia kijana anatakiwa apate muda wa kukomaa kihisia ili kukabiliana na changamoto za ukubwani.

Vijana wengi siku hizi, wanatumia taarifa ambazo hawawezi kuzikabili katika umri wao.

Ubongo unakuwa bado hauja komaa kwa shughuli hiyo yeye anakuwa tayari ameshaianza.
Akili yake, inazichukua taarifa hizo na kuzihifadhi lakini hisia zake haziko tayari kuzitumia katika namna inayopaswa.


Jamii huwa inafurahi sana kumuona kijana anajitambua na anaonyesha ishara za kukua kihisia,kwa jinsi anavyokabiliana na changamoto kubwa,katika namna inayostahili.


Kwa ufupi zifuatazo ni baadhi ya ishara (muhimu) ambazo kama kijana kwazo unaweza kuzitumia kama kipimo cha kukua kwa hisia zako;

1.KUWA MVUMILIVU





Hii ni ishara inayomtofautisha mtu ambaye amekua na yule ambaye hajakua kihisia.

Sifa moja ya watu ambao hawajakua kihisia ni kutosubiria muda muafaka wa kufanya mambo yake,yawezekana watu wengine wakaumia lakini kwa kuwa yeye amefurahi, ni sawa tu.Aliyekuwa kihisia hata kama hilo jambo ni la kumfurahisha, atasubiri tu muda muafaka ufike.



2.KUTOYUMBISHWI NA KUKOSOLEWA

Aliyekuwa kihisia anaelewa kabisa kwamba,kukosolewa ni sehemu ya kujifunza.Watu waliokua kihisia, huwa wanapokea kukosolewa bila kuruhusu ukosoaji huo uharibu mambo yake mengine.Wanajielewa wanataka nini na wao ni nani.


Na mara nyingi wanakuwa na tafsiri chanya kila wanapokosolewa,tukumbuke kuwa tumezaliwa tukiwa hatujui kila kitu kwa kila hali hivyo tunapokosolewa ni ishara ya kwamba tunachokifanya kinaonekana na kinagusa maisha ya watu.




3.WANAKUWA NA ROHO YA UNYENYEKEVU


Unyenyekevu huwa unaenda sambamba na ukuaji wa hisia.Unyenyekevu si kuwafikiria wenzako tu kwanza na wewe ukajitelekeza,hapana.Wanakuwa si watu wa kujipendelea wao tu kwa kila kitu.
Ila ni watu wa kwanza utambua kuwa uwezo waliopewa na Mungu ni kwa ajili ya viumbe na watu wanaoishi nao.


4.WANASIMAMIA MAAMUZI YAO





Wana misimamo inayotawala maamuzi yao,wako tayari kufuata misimamo yao na kupita njia ya maisha waliyochagua kwa ujasiri bila kubabaika na wanakuwa tayari kuwajibika kutokana na maamuzi yao.Tabia zao ndio zinaongoza maamuzi yao ya kila siku.


5.WEPESI WA SHUKRANI


Iko wazi kabisa, kuwa unavyozidi kukua ndio kuonyesha shukrani kwa watu na Mungu si kitu cha kuficha katika mambo madogo hadi makubwa unayofanyiwa.
Mtu ambaye hajakua anaona yote yanayomtokea anayastahili kwahiyo kushukuru hawezi.


6.KUTUMIA HEKIMA KABLA YA KUFANYA JAMBO


Mtu ambaye amekuwa anafundishika, hajioni kuwa ana majibu ya kila kitu.Jinsi anavyozidi kujua vitu ndivyo anavyozidi kutafuta hekima. Huwa hawaoni aibu kufuata ushauri kwa mwalimu, au mzazi pale anapoona amekwama.


Kd Mula anasema:: Jaribu kujichunguza, kama umekosa sifa hata moja kati ya hizo hapo juu basi ujue bado hujakua kihisia na kwa hilo nakusihi ,Usi harakie vitu ambavyo unaona kabisa muda wake bado.

Usisite kuniandikia maoni yako na pia ni vyema ukamshirikisha na mwingine nakutakia wakati mwema. 

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA