Thursday 14 September 2023

MKURUGENZI MKUU TCAA AKAGUA MABORESHO YA MRADI WA MNARA WA KUONGOZEA NDEGE UWANJA WA NDEGE MTWARA


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Hamza Johari (wa kwanza kushoto) akiongoza timu ya TCAA na Wakala wa Majengo (TBA) katika ukaguzi  mradi wa maboresho ya mnara wa kuongozea ndege unaoendelea katika Uwanja wa ndege Mtwara



Mhandisi Swalehe Nyenye kutoka TCAA akielezea mpango wa maboresho uliopo kwenye ramani ya ujenzi wa mnara huo




Timu ikiendelea kukagua hatua za mnara wa muda unaoendelea kujengwa uwanjani hapo.




Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Hamza Johari  ameongoza timu ya wataalamu kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na Wakala wa Majengo (TBA) katika ukaguzi wa  mradi wa maboresho ya mnara wa kuongozea ndege unaoendelea katika Uwanja wa ndege Mtwara.

Mradi huo unahusisha vipengele viwili ikiwa ni kujenga mnara wa muda ambapo utaruhusu waongozaji ndege kuendelea na kazi wakati mnara wa sasa ukifanyiwa maboresho unatarajiwa kukamilika kabla ya mwezi Novemba.

Huu ni muendelezo wa uboreshaji wa miundombinu unaofanywa na Serikali ya awamu ya sita katika kuhakikisha  wataalamu wanatekeleza majukumu yao katika mazingira mazuri ya kazi.



 

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA