Showing posts with label POLISI. Show all posts
Showing posts with label POLISI. Show all posts
Sunday, 21 November 2021
Saturday, 19 August 2017
MAKAMISHNA WASTAAFU POLISI WATAKIWA KUWADHIBITI WAHALIFU URAIANI
07:32 |
No Comments |
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na Kamishna Mstaafu Paul Chagonja wakati wa sherehe zilizoambatana na Gwaride maalumu la kuwaaga makamishna wastaafu watatu, gwaride lililofanyika katika viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Polisi Dar Es Salaam ambapo wastaafu hao walisukumwa kwenye gari maalumu na Makamishna Wasaidizi Waandamizi sita ikiwa ni utaratibu wa Jeshi hilo katika kuwaaga maofisa wakuu. Kulia ni Kamishna Mstaafu Hamdani Makame.
Kamishna Mstaafu Paul Chagonja akikagua gwaride maalum lililoandaliwa kwaajili ya sherehe ya kuwaaga makamishna wastaafu watatu akiwemo kamishna Chagonja, Kmaishna Paul Chagonja na Kamishna Kenneth Kaseke. Gwaride hilo lilifanyika katika viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Polisi Dar Es Salaam ambapo wastaafu hao walisukumwa kwenye gari maalumu na Makamishna Wasaidizi Waandamizi sita ikiwa ni utaratibu wa Jeshi hilo katika kuwaaga maofisa wakuu.
Makamishna wastaafu Paul Chagonja (kushoto) na Hamdani makame wakisukumwa kwenye gari na Makamishna Wasaidizi Waandamizi sita ikiwa ni utaratibu wa Jeshi la Polisi katika kuwaaga maofisa wakuu. Makamishna hao wamestaafu utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria na waliandaliwa Gwaride maalum la kuwaaga lililofanyika katika viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Polisi Dar Es Salaam. Picha kwa hisani ya Jeshi la Polisi
Na. Jeshi la Polisi.
Makamishna wastaafu wa Polisi Paul Chagonja, Hamdan Omar Makame na Kenneth Kaseke wametakiwa kuendeleza elimu ya Polisi jamii pamoja na kutoa msaada wowote utakaohitajika kwa Jeshi la Polisi pindi wanapokuwa katika maisha ya uraia baada ya kustaafu utumishi wa Jeshi la Polisi ili kuhakikisha kuwa wahalifu hawapati nafasi ya kutamba hapa nchini.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro wakati wa sherehe zilizoambatana na Gwaride maalumu la kuwaaga wastaafu hao lililofanyika katika viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Polisi Dar Es Salaam ambapo wastaafu hao walisukumwa kwenye gari maalumu na Makamishna Wasaidizi Waandamizi sita ikiwa ni utaratibu wa Jeshi hilo katika kuwaaga maofisa wakuu.
IGP Sirro alisema kazi waliyofanya wastaafu hao ni kubwa lakini kustaafu kwao siyo mwisho wa kutumika katika kazi za Polisi na hivyo waendelee kuwa tayari wakati wowote kwa kuwa sasa Jeshi la Polisi linaendelea kushirikisha jamii kukabiliana na uhalifu.
“Upolisi ni taaluma kama zilivyo taaluma nyingine hivyo utaalamu hauzeeki na kwetu sisi tunaondelea kubaki Jeshini tutaendelea kufuata yale yote mazuri mliyofanya na nyie mnapokuwa nje ya utumishi endeleeni kutusaidia kwa mawazo na milango yetu ipo wazi ili kuhakikisha nchi inaendelea kuwa salama” Alisema IGP Sirro
Akizungumza baada ya kuagwa rasmi Jeshini Kamishna Paul Chagonja ambaye alikuwa Kamishna wa Oparesheni na mafunzo kwa muda mrefu amewaasa Maofisa na Askari kuendeleza tamaduni na maadili ya Polisi pamoja na kufanya kazi kwa weledi.
Chagonja amesema nidhamu ndio msingi wa Askari Polisi popote pale wafanyapo kazi zao hivyo amewaomba kuendelea kusimamia sheria bila ya kumuonea muhali mhalifu yeyote.
Kwa upande wake Aliyekuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame amewashukuru wananchi wote hususani wa Visiwani kwa ushirikiano waliompatia kipindi chote hali ambayo imesababisha Zanzibar kuendelea kuwa shwari.
Sherehe hizo zimehudhuriwa na Viongozi mbalimbali kutoka vyombo vya ulinzi na usalama, Mkurugenzi wa Takukuru Kamishna Valentino Mlowola, IGP Mstaafu Said Mwema, DCI Mstaafu Robert Manumba na Kamishna Mstaafu wa Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam Suleiman Kova pamoja na maofisa na Askari Polisi.
Thursday, 17 August 2017
CHID BENZ AWEKWA CHINI YA UANGALIZI WA POLISI NA MAHAKAMA
12:44 |
No Comments |
Msanii Chid Benz na wenzake watano wamewekwa chini ya uangalizi maalum wa mahakama na jeshi la polisi kutokana na matumizi ya dawa za kulevya.
Chid na wenzake jana walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala baada ya upande wa Jamhuri kuiomba mahakama kuwaweka chini ya usimamizi maalum kwa kipindi cha miaka mitatu.
Polisi wa kituo cha Msimbazi waliwasilisha kiapo na kuiomba mahakama kuamuru wawekwe chini ya uangalizi maalum ikiwa ni pamoja na kusaini bondi na kuwa na wadhamini, ili kuhakikisha hawajihusishi tena na matumizi ya dawa za kulevya.
Chid na wenzake hawakuwa na pingamizi lolote kuhusu maombi hayo ya upande wa Jamhuri. Mahakama iliridhia maombi hayo na kuamuru msanii huyo na wenzake kuhakikisha wanaripoti katika kituo cha polisi cha Msimbazi mara moja kila mwezi kwa kipindi cha miaka miwili.
Aidha, kila mmoja alitakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao walitakiwa kusaini bondi ya shilingi milioni mbili kila mmoja.
Chid Benzi aliwahi kupandishwa kizimbani baada ya kukamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) miaka miwili mitatu iliyopita akiwa na kiasi kidogo cha dawa za kulevya kwenye mfuko wa shati.
Msanii huyo alikiri kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya na amewahi kuhudhuria matibabu katika jumba maalum Bagamoyo (rehab). Hivi sasa amesema ameachana na matumizi ya dawa hizo zilizomuathiri kwa kiasi kikubwa
Friday, 11 August 2017
IGP AFANYA KIKAO NA MAOFISA WA MAKAO MAKUU NA WAKUU WA VIKOSI NA VYUO
16:38 |
No Comments |
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, akitoa maelekezo kwa Maofisa Wakuu Waandamizi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi pamoja na Wakuu wa Vikosi na Vyuo vya Polisi nchini katika kikao kazi cha maelekezo kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam. Katika kikao kazi hicho IGP Sirro aliwaelekeza Maofisa hao kufanya kazi kwa weledi ili kuweza kufikia malengo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, ya kuwa na Tanzania salama isiyo na uhalifu.
Mkuu wa Utawala wa Makao Makuu ya Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Leonard Paulo, akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa kikao kazi cha Inspekta Jenerali wa polisi nchini IGP Simon Sirro na Maofisa Wakuu Waandamizi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi pamoja na Wakuu wa Vikosi na Vyuo vya Polisi nchini kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam. Katika kikao kazi hicho IGP Sirro aliwaelekeza Maofisa hao kufanya kazi kwa weledi ili kuweza kufikia malengo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, ya kuwa na Tanzania salama isiyo na uhalifu.
Picha na Jeshi La Polisi
Friday, 2 June 2017
RAIS MAGUFULI ATOA MAAGIZO MAZITO KWA IGP SIMON SIRRO
16:00 |
No Comments |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amelitaka Jeshi la Polisi nchini kutumia weledi wake kwa kiwango cha juu katika kutekeleza jukumu lake lakulinda raia na mali zao, hasa kukomesha vitendo vya uhalifu.
Mhe. Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 02 Juni, 2017wakati akizungumza na Makamanda Wakuu kutoka makao makuu ya polisi, Makamanda wa Mikoa na Vikosi vya Tanzania Bara na Zanzibar na viongozi wote wakuu wa polisi wa Mkoa wa Dar es Salaam waliokutanakatika Bwalo la Maofisa Wakuu wa polisi lililopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Mhe. Dkt. Magufuli amelipongeza Jeshi la Polisi kwa juhudi zake za kukabiliana na uhalifu lakini ametaka juhudi hizo ziongezwe hususanikukabiliana na matukio ya ujambazi na mauaji ya raia, dawa za kulevya na kuendesha operesheni zenye tija katika mikoa yote.
Amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro kujipanga vizuri yeye na safu yake ya Makamanda, Viongozi Wakuu wa Vikosi na Maofisa mbalimbali ili kuondoa dosari zote za utendaji kazi zinazoshusha ufanisi na heshima ya Jeshi la Polisi.
“Ni lazima ufanye mabadiliko makubwa, nataka kuona Jeshi la Polisi linakuwa Jeshi la Polisi, Wewe IGP Sirro na Makamnda wenzako hakikisheni mnakomesha uhalifu, komesheni mauaji dhidi ya raia, ujambazi na dawa za kulevya” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewataka Makamanda, Maofisana Askari wa jeshi hilo kujiepusha na rushwa, dawa za kulevya, kutumiwa na watu kwa maslai binafsi, kuingia mikataba isiyo na maslai kwa Jeshi na Taifa, ubadhirifu na kuacha upendeleo katika utoaji wa ajira na vyeo.
Mhe. Rais Magufuli pia ametaka Makamanda, Maofisa na Askari wote wa Jeshi la Polisi wampe ushirikiano wa kutosha IGP Simon Sirro ambaye hivi karibuni amemteua kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Mstaafu Projest Rwegasira.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
02 Juni, 2017
Mhe. Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 02 Juni, 2017wakati akizungumza na Makamanda Wakuu kutoka makao makuu ya polisi, Makamanda wa Mikoa na Vikosi vya Tanzania Bara na Zanzibar na viongozi wote wakuu wa polisi wa Mkoa wa Dar es Salaam waliokutanakatika Bwalo la Maofisa Wakuu wa polisi lililopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Mhe. Dkt. Magufuli amelipongeza Jeshi la Polisi kwa juhudi zake za kukabiliana na uhalifu lakini ametaka juhudi hizo ziongezwe hususanikukabiliana na matukio ya ujambazi na mauaji ya raia, dawa za kulevya na kuendesha operesheni zenye tija katika mikoa yote.
Amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro kujipanga vizuri yeye na safu yake ya Makamanda, Viongozi Wakuu wa Vikosi na Maofisa mbalimbali ili kuondoa dosari zote za utendaji kazi zinazoshusha ufanisi na heshima ya Jeshi la Polisi.
“Ni lazima ufanye mabadiliko makubwa, nataka kuona Jeshi la Polisi linakuwa Jeshi la Polisi, Wewe IGP Sirro na Makamnda wenzako hakikisheni mnakomesha uhalifu, komesheni mauaji dhidi ya raia, ujambazi na dawa za kulevya” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewataka Makamanda, Maofisana Askari wa jeshi hilo kujiepusha na rushwa, dawa za kulevya, kutumiwa na watu kwa maslai binafsi, kuingia mikataba isiyo na maslai kwa Jeshi na Taifa, ubadhirifu na kuacha upendeleo katika utoaji wa ajira na vyeo.
Mhe. Rais Magufuli pia ametaka Makamanda, Maofisa na Askari wote wa Jeshi la Polisi wampe ushirikiano wa kutosha IGP Simon Sirro ambaye hivi karibuni amemteua kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Mstaafu Projest Rwegasira.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
02 Juni, 2017
Thursday, 20 October 2016
DAR ES SALAAM::JESHI LA POLISI LAUA WATUHUMIWA 6 WA UJAMBAZI
09:23 |
No Comments |
Watu sita wanaotuhumiwa kuwa majambazi hatari, wameuawa katika majibizano ya risasi na Polisi katika eneo la Mbezi kwa Yusuf Makondeni katika Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Kanda Maalumu, Naibu Kamishna wa Polisi, Lucas Mkondya, watuhumiwa hao waliuawa katika majibizano ya risasi na Kikosi Maalumu cha Kupambana na Ujambazi wa Kutumia Silaha.
Mkondya alisema wamepata taarifa kutoka kwa raia mwema kuwa kuna kikundi cha watu wenye silaha, wamejipanga kufanya tukio la ujambazi kwa kutumia silaha kwa mfanyabiashara aliyekuwa akitoka Benki ya Diamond Trust Bank (DTB), tawi la Barabara ya Nyerere, ambaye angepita katika barabara hiyo kwenda mkoani Morogoro.
Alisema baada ya kupata taarifa hizo, polisi waliweka mtego na majambazi hao wakitumia gari aina ya Toyota Carina lenye namba za usajili T970 DGZ rangi ya fedha, walionekana wakilifukuza gari la mfanyabiashara huyo, kisha kulipita na kumsimamisha kwa nguvu.
“Majambazi wawili wakiwa na bastola walishuka katika gari hilo. Baada ya kugundua kuwa wameingia kwenye mtego wa polisi, walianza kufyatua risasi kwa askari wakitumia bastola na wenzao waliokuwa wamejaa kwenye gari yao walianza kushuka huku wakifyatua risasi kuelekea kwa askari,” alisema Kaimu Kamanda Mkondya.
Alisema kutokana na hali hiyo, askari walianza kujibu mashambulizi na kuwaua majambazi hao na baada ya upekuzi, zilipatikana bastola mbili, moja ya kijeshi aina ya Chinese ikiwa na risasi moja ndani ya kasha la risasi; na nyingine aina ya Browning ikiwa imefutwa namba zake na maganda sita ya risasi yaliyookotwa katika eneo la tukio.
Miili ya watuhumiwa hao imehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na upelelezi unaendelea ili kubaini mtandao mzima wa ujambazi.
Katika tukio lingine la Oktoba 17, mwaka huu saa 2:00 usiku katika maeneo ya Tegeta Masaiti, watuhumiwa watatu wa ujambazi wakiwa wamepakizana kwenye pikipiki aina ya Fekon yenye namba MC370 BEY, wakiwa na bunduki aina ya shotgun iliyokatwa mtutu na kitako, walivamia duka la Abdallah Juma (46), mkazi wa Tegeta na kupora fedha za mauzo na kuiba vocha za mitandao mbalimbali, ambazo thamani yake haijafahamika.
“Polisi baada ya kupata taarifa waliwafukuza majambazi hao, walipoona wanakaribiwa na askari, walitupa chini begi walilokuwa nalo na kutelekeza pikipiki yao kisha kukimbia, begi lilipopekuliwa lilipatikana na silaha hiyo,” alisema.
Aidha, wananchi wenye hasira waliendelea kuwakimbiza majambazi hao na kumuua mmoja huku wengine wakikimbilia kusikojulikana.
Katika hatua nyingine, Mkondya alisema wamekamata watuhumiwa wawili wa unyang’anyi kwa kutumia nguvu wakiwa na pikipiki moja na funguo bandia 75.
Katika hatua nyingine, Mkondya alisema wamekamata watuhumiwa wawili wa unyang’anyi kwa kutumia nguvu wakiwa na pikipiki moja na funguo bandia 75.
Alisema watuhumiwa hao, Ally Makwega (53) mkazi wa Tandika na Fabian Greyson (39) mkazi wa Yombo walikamatwa Oktoba 4, mwaka huu saa 6:00 usiku.
Watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na pikipiki yenye namba MC292 AMD aina ya Boxer rangi nyekundu, wanayoitumia kufanya uhalifu, wakiwa na funguo bandia 75 ambazo huzitumia katika kuvunja nyumba mbalimbali ya biashara za kulala wageni, maghala ya kuhifadhia bidhaa na maduka.
Baada ya watuhumiwa hao kuhojiwa, walikiri kuhusika na matukio mbalimbali ya uvunjaji wa maghala na kuiba katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma.
Watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.




