Showing posts with label taarifa. Show all posts
Showing posts with label taarifa. Show all posts
Sunday, 21 November 2021
Tuesday, 1 November 2016
POLISI KUTOA TAARIFA YA KIFO CHA MWANAMASUMBWI THOMAS MASHALI SIKU YA JUMATANO
08:02 |
No Comments |
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema kuwa wanaendelea na upelelezi kufuatia kuuawa kwa mwanamasumbwi Thomas Mashali na watatoa taarifa ya kifo hicho siku ya Jumatano.
Akizungumza na waandshi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro alisema taarifa zilizopo kufuatia kifo cha bondia huyo ni za kufikirika na zinasemwa tu, hivyo Jumatano atatoa taarifa hiyo.
Kamishina Sirro alisema kuwa bondia huyo ni mtu mkubwa na hakuna mtu aliethibitisha kuwa ni mny'ang'anyi, hivyo mpaka sasa ni maneno ya mtaani tu.
“Mimi ndio napata taarifa juu ya kifo cha bondia huyo. Ngoja nisubiri taarifa niweze kutoa siku ya Jumatano, ambapo nitakuwa na majibu sahihi. Kwa leo niache tu”alisema Kamishna Sirro.
Friday, 21 October 2016
WATU 6 WANASWA NA SILAHA KWA MGANGA WA KIENYEJI MWANZA
06:00 |
No Comments |
Taarifa Ya Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza Kwa Vyombo
Kwamba Tarehe 18.10.2016 Majira Ya Saa 13:00hrs Katika Eneo La Buswelu Kata Ya Buswelu Wilaya Ya Ilemela Jiji Na Mkoa Wa Mwanza, Askari Wakiwa Katika Misako Na Doria Walifanikiwa Kuwakamata Watu Sita Wakiwa Na Silaha Mbili Zilizotengenezwa Kienyeji Pamoja Na Risasi Ishirini Na Tatu, Ambazo Walikuwa Wakizitumia Katika Matukio Ya Unyang’anyi Wa Mali Na Uporaji Hapa Jijini Mwanza Na Mikoa Mingine.
Aidha Tukio Hilo Limefanikiwa Baada Ya Kupokea Taarifa Kutoka Kwa Raia Wema Kuhusu Uwepo Wa Wahalifu Hao, Ndipo Askari Walifanikiwa Kumkamata Kwanza Jeremiah Maligia @ Mkumbo Miaka 25, Mnyiramba, Fundi Seremala Mkazi Wa Malega – Singida Ambaye Alipohojiwa Alikiri Kuhusika Na Kutaja Wenzake Waliokuwa Wakishirikiana, Na Kuwa Silaha Wamezificha Kwa Mganga Wa Kienyeji Aitwaye Leornad Litta @ Makai Anayeishi Mtaa Wa Kagida – Buswelu.
Askari Walikwenda Mahali Hapo Na Kufanikiwa Kumkamata Mganga Huyo Wa Kienyeji Bwana Leornad Litta Miaka 39, Akiwa Na Silaha Hizo Mbili Zilizotengenezwa Kienyeji Hapo Nyumbani Kwake Na Risasi Ishirini Na Mbili Zinazotumiwa Na Bunduki Ya Aina Ya Short Gun Na Risasi Moja Ya Rifle Aina Ya Mark Iv.
Aidha Katika Kuhojiwa Zaidi Na Askari Watuhumiwa Tajwa Hapo Juu Waliwataja Washirika Wao Wanne Ambao Walikuwa Wakishirikiana Katika Kufanya Uhalifu Ambapo Askari Walifanikiwa Kuwakamata, Ambao Ni 1. Kamgisha Jovini Kamhambwa Miaka 40, Mlinzi Na Mkazi Wa Iloganzala, 2. Juma Yusuph @ Jimi Miaka 35, Mkazi Wa Bwani Kinondoni, 3. Samweli Peter Miaka 36, Mkazi Wa Busweli Na 4. Shabani Hussein Miaka 26, Fundi Viatu Na Mkazi Wa Nyasaka Msumbiji.
Watuhumiwa Wote Walipofanyiwa Mahojiano Walikiri Kwamba Silaha Hizo Walizitumia Katika Unyang’anyi Wa Mali Na Uporaji Katika Maeneo Ya Jiji Na Mkoa Wa Mwanza, Aidha Jeshi La Polisi Kwa Sasa Linaendelea Na Uchunguzi Kuhusiana Na Tukio Hilo Na Matukio Waliyokuwa Wameyafanya, Pindi Uchunguzi Ukikamilika Watuhumiwa Wote Watafikishwa Mahakamani.
Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Mwanza Naibu Kamishina Wa Polisi Ahmed Msangi Anatoa Wito Kwa Wakazi Wa Jiji Na Mkoa Wa Mwanza Akiwataka Kuendelea Na Tabia Ya Kutoa Ushirikiano Kwa Jeshi Lao La Polisi, Ili Tuweze Kudhibiti Uhalifu Katika Mkoa Wetu., Lakini Pia Anatoa Angalizo Kwa Wananchi Haswa Vijana Akiwataka Kuacha
Tabia Ya Kujihusisha Na Uhalifu Bali Wajikite Katika Kufanya Shughuli Halali Za Maendeleo, Kwani Jeshi La Polisi Lipo Vizuri
Kuhakikisha Ulinzi Na Usalama Upo Kwa Raia Wote Wa Jiji Na Mkoa Wa Mwanza.
Katika Tukio La Pili
Mnamo Tarehe 18.10.2016 Majira Ya Saa 14:00hrs Mchana Katika Eneo La Ilemela Wilaya Ya Ilemela Jiji Na Mkoa Wa Mwanza, Askari Walifanikiwa Kuwakamata Watu Wawili Ambao Ni 1. Rahim Feka Miaka 28, Mkazi Wa Ilala – Dar Es Salaam, 2. Ally Kawalale Miaka 32, Mkazi Wa Jetrumo – Arport Dar Es Salaam, Wakiwa Wanataka Kuuza Gari Lenye Namba T.778 Azv Aina Ya Toyota Land Cruiser Lililokuwa Wameliiba Huko Ilala Jijini Dar Es Salaam.
Aidha Watuhumiwa Hao Walikamatwa Baada Ya Kupokelewa Taarifa Ya Kuibiwa Kwa Gari Hilo Huko Dar Es Salaam Na Kwamba Kuna Uwezekano Kuwepo Eneo La Kanda Ya Ziwa, Ndipo Ulifanyika Upelelzi Kuhusiana Na Taarifa Hiyo, Na Kufanikiwa Kuwakamata Watuhumiwa Tajwa Hapo Juu Wakiwa Na Gari Hilo.
Watuhumiwa Wote Wapo Chini Ya Ulinzi Wa Jeshi La Polisi Wakiendelea Na Mahojiano , Huku Taratibu Za Kuwasafirisha Kwenda Dar Es Salaam Wakiwa Chini Ya Ulinzi Wa Askari Polisi Zikiwa Bado Zinaendelea.
Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Mwanza Naibu Kamishina Wa Polisi Ahmed Msangi Anatoa Rai Kwa Wakazi Wa Jiji Na Mkoa Wa Mwanza Akiwataka Kuacha Tabia Ya Kununua Vitu Vya Wizi, Bali Pindi Wanapoona Biashara Za Wizi Zinataka Kufanyika Au Zinafanyika Watoe Taarifa Polisi Ili Watuhumiwa Waweze Kukamatwa Na Kufikishwa Mahakamani.
Katika Tukio La Tatu
Kwamba Tarehe 18.10.2016 Majira Ya Saa 23:00hrs Katika Kitongoji Cha Ibungiro Kijiji Cha Sagani Kata Ya Kandawe Wilaya Ya Magu Mkoa Wa Mwanza, Mtu Mmoja Msichana Aliyejulikana Kwa Jina La Dema Charles @ Bulayi Miaka 20, Mkazi Wa Kandawe, Ameuawa Kwa Kukatwa Na Vitu Vyenye Ncha Kali Sehemu Za Kichwani Na Kiunoni
Akiwa Amelalala Na Watu Wasiojulikana, Huku Wenzake Wa Wili Wakijeruhiwa Sehemu Mbalimbali Za Miili Yao.
Majeruhi Waliojeruhiwa Katika Tukio Hilo Ni 1.mariam Lucas @ Kapele Miaka 26, Mkazi Wa Kijiji Cha Sagani Aliyejeruhiwa Shingoni Na Kwenye Kiganja Cha Mkono Wa Kulia, 2. Kapelele Makubi @ Salulo Miaka 90, Ambaye Ni Baba Mwenye Nyumba/ Mji, Aliyejeruhiwa Mgongoni, Kichwani Na Kiunoni.
Inadaiwa Kuwa Wauaji Hao Walifika Katika Nyumba Hiyo Majira Tajwa Hapo Juu Na Kuwakuta Wenye Mji Wakiwa Wamelala, Ndipo Waliingia Ndani Na Kufanya Mauaji Hayo, Hadi Sasa Hakuna Mtu Yeyote Aliyekamatwa Kuhusiana Na Tukio Hilo.
Aidha Uchunguzi Wa Awali Umebainisha Kuwa Mauji Hayo Yametokana Na Kulipiza Kisasi, Jeshi La Polisi Kwa Sasa Lipo Katika Upelezi Pamoja Na Uchunguzi Kuhusiana Na Tukio Hilo, Majeruhi Wapo Katika Hospitali Ya Wilaya Ya Magu Wakiendelea Kupatiwa Matibabu Na Hali Zao Zinaendelea Vizuri.
Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Mwanza Naibu Kamishina Wa Polisi Ahmed Msangi Anatoa Wito Kwa Wakazi Wa Jiji Na Mkoa Wa Mwanza Akiwataka Kutoa Ushirikiano Kwa Jeshi La Polisi Ili Watuhumiwa Wa Mauaji Hayo Wawezwe Kukamatwa Na Kufikishwa Katika Vyombo Vya Sheria.
Imetolewa Na:
Dcp: Ahmed Msangi
Kamanda Wa Polisi (M) Mwanza
Thursday, 20 October 2016
DAR ES SALAAM::JESHI LA POLISI LAUA WATUHUMIWA 6 WA UJAMBAZI
09:23 |
No Comments |
Watu sita wanaotuhumiwa kuwa majambazi hatari, wameuawa katika majibizano ya risasi na Polisi katika eneo la Mbezi kwa Yusuf Makondeni katika Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Kanda Maalumu, Naibu Kamishna wa Polisi, Lucas Mkondya, watuhumiwa hao waliuawa katika majibizano ya risasi na Kikosi Maalumu cha Kupambana na Ujambazi wa Kutumia Silaha.
Mkondya alisema wamepata taarifa kutoka kwa raia mwema kuwa kuna kikundi cha watu wenye silaha, wamejipanga kufanya tukio la ujambazi kwa kutumia silaha kwa mfanyabiashara aliyekuwa akitoka Benki ya Diamond Trust Bank (DTB), tawi la Barabara ya Nyerere, ambaye angepita katika barabara hiyo kwenda mkoani Morogoro.
Alisema baada ya kupata taarifa hizo, polisi waliweka mtego na majambazi hao wakitumia gari aina ya Toyota Carina lenye namba za usajili T970 DGZ rangi ya fedha, walionekana wakilifukuza gari la mfanyabiashara huyo, kisha kulipita na kumsimamisha kwa nguvu.
“Majambazi wawili wakiwa na bastola walishuka katika gari hilo. Baada ya kugundua kuwa wameingia kwenye mtego wa polisi, walianza kufyatua risasi kwa askari wakitumia bastola na wenzao waliokuwa wamejaa kwenye gari yao walianza kushuka huku wakifyatua risasi kuelekea kwa askari,” alisema Kaimu Kamanda Mkondya.
Alisema kutokana na hali hiyo, askari walianza kujibu mashambulizi na kuwaua majambazi hao na baada ya upekuzi, zilipatikana bastola mbili, moja ya kijeshi aina ya Chinese ikiwa na risasi moja ndani ya kasha la risasi; na nyingine aina ya Browning ikiwa imefutwa namba zake na maganda sita ya risasi yaliyookotwa katika eneo la tukio.
Miili ya watuhumiwa hao imehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na upelelezi unaendelea ili kubaini mtandao mzima wa ujambazi.
Katika tukio lingine la Oktoba 17, mwaka huu saa 2:00 usiku katika maeneo ya Tegeta Masaiti, watuhumiwa watatu wa ujambazi wakiwa wamepakizana kwenye pikipiki aina ya Fekon yenye namba MC370 BEY, wakiwa na bunduki aina ya shotgun iliyokatwa mtutu na kitako, walivamia duka la Abdallah Juma (46), mkazi wa Tegeta na kupora fedha za mauzo na kuiba vocha za mitandao mbalimbali, ambazo thamani yake haijafahamika.
“Polisi baada ya kupata taarifa waliwafukuza majambazi hao, walipoona wanakaribiwa na askari, walitupa chini begi walilokuwa nalo na kutelekeza pikipiki yao kisha kukimbia, begi lilipopekuliwa lilipatikana na silaha hiyo,” alisema.
Aidha, wananchi wenye hasira waliendelea kuwakimbiza majambazi hao na kumuua mmoja huku wengine wakikimbilia kusikojulikana.
Katika hatua nyingine, Mkondya alisema wamekamata watuhumiwa wawili wa unyang’anyi kwa kutumia nguvu wakiwa na pikipiki moja na funguo bandia 75.
Katika hatua nyingine, Mkondya alisema wamekamata watuhumiwa wawili wa unyang’anyi kwa kutumia nguvu wakiwa na pikipiki moja na funguo bandia 75.
Alisema watuhumiwa hao, Ally Makwega (53) mkazi wa Tandika na Fabian Greyson (39) mkazi wa Yombo walikamatwa Oktoba 4, mwaka huu saa 6:00 usiku.
Watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na pikipiki yenye namba MC292 AMD aina ya Boxer rangi nyekundu, wanayoitumia kufanya uhalifu, wakiwa na funguo bandia 75 ambazo huzitumia katika kuvunja nyumba mbalimbali ya biashara za kulala wageni, maghala ya kuhifadhia bidhaa na maduka.
Baada ya watuhumiwa hao kuhojiwa, walikiri kuhusika na matukio mbalimbali ya uvunjaji wa maghala na kuiba katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma.
Watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
Wednesday, 5 October 2016
Monday, 22 August 2016
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
15:30 |
No Comments |
Katika siku za hivi karibuni, kumekuwepo na mitazamo tofauti miongoni mwa jamii kufuatia kuonekana kwa askari polisi wakifanya mazoezi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Kufuatia hali hiyo, jeshi la polisi nchini, linatumia fursa hii kuwatoa hofu wananchi kwamba mazoezi hayo ni ya kawaida kwa askari wa jeshi la polisi
Aidha, jeshi la polisi linawataka wananchi kuendelea na shughuli zao za kawaida kwa sababu mazoezi hayo hayalengi kuzuia shughuli zozote halali zinazofanywa na wananchi.
Imetolewa na:
Advera John Bulimba – Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP)
Msemaji wa Jeshi la Polisi,
Makao Makuu ya Polisi.
Friday, 12 August 2016
Thursday, 11 August 2016
TAARIFA TOKA IKULU KUHUSU ZIARA YA RAIS MAGUFULI JIJINI MWANZA ILIYOANZA JANA
08:30 |
No Comments |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 10 Agosti, 2016 ameanza ziara ya siku mbili katika mikoa ya Geita na Mwanza baada ya kumaliza mapumziko mafupi nyumbani kwake Chato Mkoani Geita.
Jijini Mwanza Rais Magufuli alipokelewa na maelfu ya wananchi waliokuwa wakisimamisha msafara wake tangu alipoingia kupitia kivuko cha Busisi - Kigongo na baadaye kupita Usagara, Buhongwa, Mkolani, Nyegezi, Mkuyuni na Igogo ambako pamoja na kuwahakikishia kuwa Serikali yake imejipanga kukabiliana na kero mbalimbali za wananchi na kuwaletea maendeleo, amesitisha agizo la Jiji la Mwanza la kuwataka wafanyabiashara wadogo maarufu kwa jina la Machinga kutofanya biashara zao katikati ya Jiji ifikapo tarehe 20 Agosti, 2016.
Pamoja na kusitisha agizo hilo, Dkt. Magufuli amewaagiza viongozi wa Jiji la Mwanza na Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kutafuta na kuandaa maeneo ambayo wafanyabiashara hao watayatumia kwa ajili ya kufanyia biashara zao.
"Na mtakapowatafutia maeneo ya biashara wapelekeni sehemu ambazo ni nzuri, msiwapeleke sehemu ambazo hazina biashara, hawa wamachinga wanaendesha maisha yao kwa kutumia biashara hizi"Amesema Rais Magufuli.
Aidha, Rais Magufuli amewahakikishia wananchi wa Mwanza kuwa Serikali imeanza kufanya usanifu na upembuzi yakinifu ikiwa ni maandalizi ya kuanza ujenzi wa daraja kubwa litakalounganisha eneo la Busisi Wilayani Sengerema na Kigongo Wilayani Misungwi ili kuondoa adha ya wananchi kuvuka eneo hilo kwa kutegemea vivuko, na pia itahakikisha inanunua meli moja katika ziwa viktoria kama ilivyoahidi.
Kabla ya kuingia Jijini Mwanza Rais Magufuli alihutubia mkutano wa hadhara katika Mji wa Sengerema na pia alizungumza na wananchi wa Sima Wilayani Sengerema na Kasamwa Wilayani Geita ambako aliwahakikishia kuwa Serikali yake itaongeza msukumo katika kutatua tatizo la uhaba wa maji katika maeneo hayo kwa kusambaza maji ya kutoka ziwa Viktoria huku akiwataka viongozi halmashauri husika kutumia rasilimali za halmashauri kutatua tatizo hilo la maji katika maeneo ambayo hayatapitiwa na mradi mkubwa wa maji ya kutoka ziwa Viktoria.
Katika hatua nyingine Mhe. Rais Magufuli amewaagiza viongozi wa Mikoa ya Mwanza na Geita kutafakari sababu zilizosababisha kufa kwa Chama Kikuu cha Ushirika cha NYANZA na viwanda vya kuchambua pamba (Ginneries) ili kupanga namna ya kuvifufua.
Rais Magufuli alitoa agizo hilo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kasamwa kilichopo Wilayani Geita na ameahidi kuwa Serikali yake ipo tayari kuunga mkono juhudi za wakulima kwa kuanzisha viwanda vya kuongeza thamani ya mazao yao ikiwemo zao la pamba.
Rais Magufuli atakamilisha ziara yake ya siku mbili leo tarehe 11 Agosti, 2016 kwa kuweka jiwe la msingi katika Daraja la watembea kwa miguu na kuzungumza na wananchi wa Mwanza katika Uwanja wa Furahisha.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Mwanza
10 Agosti, 2016
Thursday, 21 July 2016
Tuesday, 19 July 2016
FEDHA ZA MAFUNZO KWA VITENDO KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU KUTOKA BODI YA MIKOPO KUTOLEWA BAADA YA UHAKIKI WA WANAFUNZI HEWA
20:58 |
No Comments |
Na: Lilian Lundo – MAELEZO
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameeleza kuwa fedha kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo zitatolewa mara baada ya kukamilika kwa zoezi la uhakiki wa wanafunzi waliombewa fedha hizo toka vyuo mbalimbali hapa nchini.
Prof. Ndalichako aliyasema hayo leo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa ufafanuzi juu ya ucheleweshwaji wa fedha hizo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu.
“Kuna zaidi ya wanafunzi 2,736 hewa ambao majina yao yamewasilishwa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kwa ajili ya kulipwa fedha za mafunzo kwa vitendo, yakiwemo majina ya wanafunzi waliofariki na waliofukuzwa chuo,” alifafanua Prof. Ndalichako.
Aliendelea kwa kusema kuwa, kuna chuo ambacho kilituma ripoti ya wanafunzi waliofukuzwa chuo mwaka 2013/2014 lakini majina hayo yametumwa tena kwa ajili ya kupewa fedha za mafunzo kwa vitendo kwa mwaka huu.
Kutokana na kasoro zilizojitokeza katika majina ya wanafunzi wanaotakiwa kupewa fedha kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo Prof. Ndalichako amesema kuwa Serikali haitatoa fedha mpaka uhakiki wa wanafunzi wanaotakiwa kupata fedha hizo utakapo kamilika kwa vyuo vyote nchini.
Aidha, Mhe. Ndalichako amesema kuwa majina ya wanafunzi hao hewa yamewekwa katika mitandao wakitakiwa kujihakiki TCU ili kujiridhisha kama kweli ni wanafunzi na wanaendelea na masomo.
Vile vile, Prof. Ndalichako amevitaka vyuo vikuu kutoa ushirikiano kwa timu zilizotumwa katika vyuo vyao kufanya uhakiki wa wanafunzi wanaotakiwa kupata fedha hizo kwani kuna baadhi ya vyuo vimekuwa havitoi ushirikiano kwa kisingizio cha kuwepo kwenye mitihani.
Aliongeza kwa kusema kuwa, vyuo kutotoa ushirikiano kwa timu zilizotumwa kufanya uhakiki wa wanafunzi hao kutazidi kuchelewesha fedha hizo kutoka mapema.
Tuesday, 17 May 2016
MAENEO YA JIJI LA DAR ES SALAAM NA BAGAMOYO KUKOSA MAJI KWA SAA 10
19:53 |
No Comments |
TAARIFA
KWA UMMA
17/5/2016
KUZIMWA
KWA MTAMBO WA RUVU CHINI
Shirika
la Maji Safi na Majitaka Dar-es-salaam (DAWASCO),
linawatangazia wakazi wa jiji la
Dar-es-salaam pamoja na Mji wa Bagamoyo kuwa Mtambo wa kuzalisha Maji
wa Ruvu Chini utazimwa kwa wastani wa Saa 10 kuanzia saa 5 asubuhi Jumanne,
Tarehe 17/05/2016.
Sababu za kuzimwa kwa
Mtambo wa Ruvu Chini ni kuzuia uvujaji uliotokea mtamboni kwenye bomba la inchi
72.
Kuzimwa
kwa mtambo wa Ruvu Chini kutasababisha maeneo yafuatayo katika Jiji la Dar es
salaam kukosa Maji:
MJI WA BAGAMOYO
VIJIJI VYA ZINGA, KEREGE NA MAPINGA, BUNJU, BOKO, TEGETA, KUNDUCHI, SALASALA,
JANGWANI, MBEZI BEACH NA KAWE.
Maeneo Mengine ni :
MLALAKUWA, MWENGE,
MIKOCHENI, MSASANI, SINZA, KIJITONYAMA, KINONDONI, OYSTERBAY, MAGOMENI, UPANGA,
KARIAKOO, CITY CENTRE, ILALA, UBUNGO MAZIWA, KIGOGO, MBURAHATI, HOSPITALI YA
RUFAA MUHIMBILI, BUGURUNI, CHANGOMBE NA KEKO.
WANANCHI
MNASHAURIWA KUHIFADHI MAJI NA KUYATUMIA KWA MATUMIZI YA LAZIMA.
DAWASCO INAWAOMBA RADHI WANANCHI WA MAENEO HUSIKA
KWA USUMBUFU UTAKAOJITOKEZA.
Wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja
022-2194800 au 0800110064 (BURE)
IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
DAWASCO-MAKAO MAKUU








