ASKOFU WA KANISA LA KKKT LILILOLIPULIWA BOMU JIJINI MWANZA ATOA KAULI NZITO
Miongoni
mwa habari kubwa wiki hii ni hii ya bomu kulipuliwa kwenye kanisa la
kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) Mwanza ambapo lilijeruhi mtu mmoja
alielazwa hospitali ya Bugando.
Mkuu wa
dayosisi Askofu Andrew Gulle anasema: "May 5 2014 bomu limelipuka katika
usharika wa kanisa kuu Imani kwenye eneo la rest house saa mbili usiku,
ni bomu la kutengenezwa kwa mkono na lilikua limewekwa kwenye karatasi
za kufungia zawadi na kuwekwa kwenye mfuko wa plastiki na kuwekwa kwenye
varanda ya rest house yetu.
"Kifurushi
hicho kimekuwepo kuanzia siku ya Ijumaa ambapo ilipofika Jumatatu saa
mbili usiku muhudumu wa rest house Benadertha alianza kujiuliza
kifurushi hicho kina nini na kwanini kimekuwepo hapo kwa siku tatu?
ambapo mwishowe aliamua kukifungua ili kujua kuna nini ndani lakini
ghafla bomu lililipuka kwa kishindo na moshi mwingi huku likisambaza
misumari midogomidogo na kumjeruhi miguuni na usoni..
"Alikimbizwa hospitali ya rufaa ya Bugando na kufanyiwa upasuaji na
kulazwa kwenye wodi ya mifupa, hatujui lengo la wahusika lilikua
kumuumiza yeye au wengi zaidi, au walishindwa kulifikisha walipotaka
lifike?
"Vikao vya kanisa vimekaa kutafakari na sasa natamka kama kiongozi wa Dayosisi yale tuliyokubaliana kuyasema kwa Watanzania……
"Tunalaani kitendo hicho kilichofanyika kwenye eneo la Kanisa,
tunaomba makanisa yetu kuboresha ulinzi katika maeneo yetu yote maana
kwa sababu hatuwezi kujua watu hawa wamekusudia kuweka mabomu wapi na
wapi.
"Tunaomba serikali ihakikishe inawashika waliohusika na kutokomeza
mtandao huu wa ugaidi kabla haujaota mizizi na kuhatarisha amani
tuliyoizoea Tanzania.
"Mwisho tunatoa wito kwa Wakristo wote wawe
watulivu, wasiogope wala wasitishwe na mashambulizi yanayotendeka,
tunatoa wito kwa Wakristo wote kwamba kusitokee fujo popote wala
kulipiza kisasi, silaha yetu kubwa ni maombi na kumtegemea Mungu, wakati
huu kanisa linapoteswa ndio wakati wa kumtegemea Mungu zaidi na
kuhubiri habari njema"
0 comments:
Post a Comment