Kanda ya ngono yamtia mashakani mwalimu mkuu
Shule iliyokumbwa na kashfa
Mwalimu mkuu wa shule moja ya
upili nchini Uingereza ameachishwa kazi kufuatia utata kuhusu kanda ya
ngono inayodaiwa kurekodiwa shuleni humo.
Mwenyekiti wa bodi ya shule alimwachisha kazi
mwa muda mwalimu mkuu Graham Daniels na mfanyakazi mwingine wa shule
ambaye jina lake halikutajwa baada ya malalamiko kutolewa kuwahusu
wawili hao.Hata hivyo wakuu wa bodi walisema kuwa shughuli za masomo zinaendelea kama kawaida.
Mkuu wa bodi alisema: "shule imepokea malalamiko ambayo hayakumtaja mtu yeyote lakini kufuatia madai hayo uchunguzi utafanywa.''
Mwalimu mkuu na mfanyakazi mwingine wa shule wameachishwa kazi kutokana na madai hayo.
na BBC
0 comments:
Post a Comment