KITUKO: MENO YA TEMBO YAIBWA KATIKA KITUO CHA POLISI
Polisi akilinda sehemu ya shehena ya meno ya tembo iliyokamatwa Dar es Salaam hivi karibuni. Picha ya Maktaba
Meno ya tembo yaliyohifadhiwa kwa ajili ya vielelezo mahakamani yalitoweka katika Kituo cha Polisi cha Kilwa mkoani Lindi. Tukio
hilo limenukuliwa katika Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
za Serikali (CAG), ikisema meno makubwa 108 ya tembo na kilo 20 za meno
mengine ya tembo yaliyokuwa yamehifadhiwa kama kielelezo cha kesi za
uhujumu uchumi, yamebainika kutoweka kinyemela.Ripoti
hiyo iliyowasilishwa bungeni juzi, imebainisha kuwa meno mengine
makubwa ya tembo yaliyokuwa na uzito wa kilo 498.3 yamebadilishwa
kinyemela na meno madogo, hivyo kusababisha hasara ya kilo 203.66 za
meno ya tembo ambazo thamani yake haikufahamika.CAG
Ludovick Utouh katika ripoti hiyo ya mwaka ulioishia Juni 30, 2013,
amebainisha kuwa kumbukumbu katika Pori Tengefu la Miguruwe zilionyesha
kuwa katika kipindi cha kuanzia Juni 5 hadi Juni 8, 2012 meno makubwa
108 yalikuwa miongoni mwa vielelezo kituoni hapo.Kati
ya meno hayo 108 yaliyokamatwa katika matukio ya ujangili, 74
yalitoweka katika kituo cha polisi wakati 34 yalibadilishwa na meno
madogo, tofauti na yale yaliyokuwa yamekamatwa yakihusishwa na kesi ya
ujangili Na. 3/2009 na kesi nyingine ya uhujumu uchumi Na. 2/2010 ambazo
zilikuwa zikiendelea mahakamani mkoani Lindi.
Pia
ilibainika kuwa kilo 20 za meno ya tembo ambayo yalikamatwa na
kuhifadhiwa kama kielelezo cha majalada KLM/IR/184/2009, KLM/IR/235/2009
na KLM/IR/567/2010 yalitoweka.
Gari la ujangili latowekaUkaguzi
huo pia ulibaini kuwa gari lililokamatwa likiwa kielelezo baada ya
kukutwa na kilo 26 za meno ya tembo yenye thamani ya Sh135 milioni
liliondolewa kinyemela katika Kituo cha Polisi Kilwa.CAG
katika ukaguzi huo alibaini upungufu katika usimamizi wa meno ya tembo
na nyara nyingine za taifa katika chumba cha meno hayo Dar es Salaam na
vituo vya mikoani.CAG
katika taarifa yake hiyo amesema kutokana na kukosekana kwa kumbukumbu
sahihi, meno ya tembo yanaweza kuibwa au kupotea bila menejimenti kuwa
na taarifa yoyote, hivyo ameishauri Serikali kuhakikisha kunakuwa na
udhibiti wa kutosha katika usimamizi wa nyara za Serikali nchi nzima.
MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment