KOCHA WA EVERTO (MARTINEZ) ATAKA SHERIA YA MIKATABA YA MKOPO KWA WACHEZAJI IBADILISHWE
KOCHA
wa Everton, Roberto Martinez ameomba sheria ya wachezaji wa mkopo
ifanyiwe marekebisho na kuwaruhusu kucheza dhidi ya klabu walizotoka.
Martinez
ameweza kuwatumia vizuri wachezaji wake wa mkopo akiwa Goodison Park,
Romelu Lukaku, Gerard Deulofeu na Gareth Barry na wote wamekuwa katika
kiwango cha kuvutia katika klabu hiyo ya Merseyside.
Kocha
huyo atamkosa Barry jamamosi kwenye mchezo dhidi ya Manchester City
kwasababu sheria ya mkopo haimruhusu kucheza na klabu yake inayommiliki.
Kocha
huyo wa zamani wa Wigan Athletic amesema imefika wakati watu wa sheria
za ligi kuu nchini England waliangalie hilo, huku akionesha mfano jinsi
Atletico Madrid walivyomtumia Thibaut Courtois dhidi ya mwajiri wake wa
kudumu, klabu ya Chelsea kwenye mechi za nusu fainali za UEFA.
“Unapofikia makubaliano ya kumtoa mchezaji kwa mkopo, aruhusiwe kucheza”. Martinez alisema.
“Sioni kama ni haki kumnyima mchezaji haki ya kucheza na klabu yake aliyomwajiri”.
“Ni
haki kufanya kama ilivyo katika mashindano ya ulaya, kumuona mchezaji
akicheza na timu yake iliyomwajiri ni jambo zuri na nadhani itakuwa
jambo la maana na baada ya msimu ataangaliwa kiwango chake”.
“Sheria ya mkopo inahitaji mabadiliko ili kuendana na soka la kisasa. Ni mjadala mzuri na ni jambo la kuangaliwa kwa ndani”.
“Hatupaswi
kuwa na sheria mbili tofauti katika mashindano. Nadhani sheria za ligi
ya ndani ziende sambamba na sheria michuano ya ulaya”.
0 comments:
Post a Comment