RAIS KIKWETE AKUTANA NA MFANYABIASHARA MAARUFU WA NIGERIA ALHAJ ALIKO DANGOTE JIJINI ABUJA

Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na mfanyabishara
maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote alipokutana naye jijini Abuja,
Nigeria, May 8, 2014 pembeni mwa Mkutano wa Dunia wa Uchumi kwa Afrika.
Alhaj Dangote ni mwekezaji mashuhuri duniani na hivi sasa anajenga
kiwanda kikubwa cha saruji mkoani Mtwara.

Mfanyabishara
maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote akisalimiana na Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Bi. Juliet Kairuki wakati
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete alipokutana kwa mazungumzo na
mfanyabishara huyo maarufu wa Nigeria jijini Abuja, Nigeria, May 8, 2014
pembeni mwa Mkutano wa Dunia wa Uchumi kwa Afrika.

Rais Dkt
Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono baada ya mazungumzo na
mfanyabishara maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote alipokutana naye
jijini Abuja, Nigeria, May 8, 2014.PICHA NA IKULU
0 comments:
Post a Comment