Tuesday 19 May 2015

WESTBROMWICH YAITIA DOA CHELSEA



West Brom imewachabanga mabingwa ligi kuu ya England Chelsea jumla ya mabao 3-0 hali ambayo kwa sasa inaifanya klabu hiyo kukaa eneo salama zaidi dhidi ya kushuka daraja.
Katika mechi hiyo iliyochezwa, dimba la The Hawthons, Saido Berahino alikata utepe wa magoli kwa kufunga goli la kwanza mnamo dakika ya 9,na pia dakika ya 47 Berahino tena akaweka kimiani goli la pili kwa njia ya penati ,baada ya kuangushwa na John Terry eneo la adhabu na hivyo hadi mwisho wa mchezo West Brom 3 Chelsea mabingwa nunge. Kwa matokeo hayo West Brom sasa wamefanikiwa kukaa eneo salama kuepuka kushuka daraja,huku Chelsea wakiwa bado mabingwa. Kesho Arsenal watakwaana na Sunderland

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA