BARCELONA BINGWA ULAYA, YAIPIGA JUVENTUS 3-1,
Mabao ya Raktic katika kipindi cha kwanza, Luis Suarez na Neymar katika kipindi cha pili yameiwezesha Barcelona kuibuka mabingwa wa Ulaya kwa kuichapa Juventus bao 3-1.
Bao pekee la Moratta halikuweza kuiokoa Juventus iliyocheza mpira wa ushindani na kuipa Barcelona ushindani mkubwa.
Fainali hiyo kwenye Uwanja wa Berlin, Ujerumani, ilikuwa ni ya kuvutia, ya ushindani na kivutio kikubwa.
0 comments:
Post a Comment